DSTV bado inafanya vizuri na ukizingatia haina mipaka ndani ya Tanzania
na ndo sababu ya kukufanya popote ulipo unaweza kufunga na ukaona kila
ambacho unapaswa kuona kutokana na Package uliyoilipia!!
Kwa mantiki hiyo ikafanya watu watoke sehemu moja inaitwa IKWIRIRI na kutaka nikawafungie DSTV ili wacheck mipira na mengine ya kupendeza ila kubwa likiwa mipira,nami si nipo kwa ajili ya kufurahisha wengine huku mkono ukienda kinywani nikasababisha kama ambavyo unaona mwanaume hasifiwi sura!!
Hapa kazi tu!!
Safari ilikuwa ni ya siku moja tu,nimetoka Dar mchana nikafika kule jioni nikapumzika kisha siku inayofuata asubuhi nikafanya kilichonipeleka nilipomaliza nikatembea tembea kidogo kuona IKWIRIRI ilivyo maana ndo mara ya kwanza kufika ila ambacho naweza kusema pazuri banaa nimepapenda kiasi kwamba hata kuweka kambi naweza kwasababu ni mjini na mji ndo unakua!!
Nnachofurahi kwangu safari moja huanzisha nyengine na ndo kilichotokea Mungu akipenda ntakuwepo tena next week,umuhimu wangu umeonekana hivyo nnahitajika kurudi!!
Nnachofurahi kwangu safari moja huanzisha nyengine na ndo kilichotokea Mungu akipenda ntakuwepo tena next week,umuhimu wangu umeonekana hivyo nnahitajika kurudi!!