Call / WhatsApp +255673378129

Nov 1, 2013

TING WAMEHAMA SATELLITE


Niliwahi kuwaambia baadhi ya watu ila ikawa kama hawanielewi hivi baada ya kukataa kuwafungia local channels kupitia Dish dogo baada kugundua kama hizo local uhai wake mdogo,kwa maana satellite waliyokuwa wamewekwa na Ting kwa lugha nyepesi ilikuwa ni mali ya Ting!!
Awali Ting walikuwa Eutelsat 36A degree 36.0E,ambapo walikuwa sawa na Dstv wale wadau watakuwa wanakumbuka kwakuwa ilikuwa unaweza ukatumia Dish moja kwa kupata Ting na Dstv!!
Sasa wamehamia Amos 5 degree 17.0E wala sio mbali saaana na ilipokuwa awali!
Kama wewe ni fundi haya!
Satellite: Amos 5 - 17 degrees East
Frequency: 12417Mhz
Symbol Rate: 30000Msps
Modulation: 8 PSK
FEC : 2/3
Pilots On
Share:

Oct 23, 2013

AZAM TV

Mustapha MaDish  nikiwa Azam tv HQ
Niseme tu ukweli katika ujio wa ving'amuzi vyote Tanzania huu ni ujio tofauti sana,kwa maana kabla ya kuanza kuuza wadau wamekuwa na shauku ya kutaka kununua bila kujua nini kilichopo ila tu wanaamini itakuwa king'amuzi bora kuliko ving'amuzi vyote vilivyopo Tanzania ukiweka mbali wakongwe Dstv,sababu kubwa ikiwa ni mmiliki wa hii kampuni kwa kuwa muda mrefu katika biashara si ya ving'amuzi ila biashara nyengine na sifa yake kuu bidhaa bora kwa bei nafuu,hivyo imani ya watanzania ni kwamba unafuu unakuja!!
Swali je Azam tv ni bei rahisi kweli ama magumashi!!??
VIFAA NI TSH 135000/= BILA UFUNDI
Kujua vifurushi Bofya Hapa
Mustapha MaDish kwa site!

Hapa milele

 Mkataba

 Burudani kwa wote

 Sehemu sahihi ya wewe kuhudumiwa

 Mwendo ule ule

 Mustapha MaDish ameshafanya yake
Niseme tu ukweli katika ujio wa ving'amuzi vyote Tanzania huu ni ujio tofauti sana,kwa maana hawajaanza kuuza isipokuwa wadau wamekuwa na shauku ya kutaka kununua bila kujua nini kilichopo ila tu wanaamini itakuwa king'amuzi bora kuliko ving'amuzi vyote vilivyopo Tanzania ukiweka mbali wakongwe Dstv,sababu kubwa ikiwa ni mmiliki wa hii kampuni kwa kuwa muda mrefu katika biashara si ya ving'amuzi ila biashara nyengine na sifa yake kuu bidhaa bora kwa bei nafuu!!
Swali je Azam tv ni bei rahisi kweli ama magumashi!!??
Bei ni Tsh.135000/= Unapata Dish,Decoder.lnb,Cable 
hii inakuwa haina kufungiwa na kufungiwa ni tsh 30,000/=
Baada ya hapo unachagua vifurushi ili upate vifurushi Bofya Hapa

  Haya kazi ni kwako je ni rahisi ama ghari!!??
Ila mi nilichopenda kutumia Dish tofauti na baadhi ya ving'amuzi vyengine wanaotumia Antenna hii inamaanisha watakuwepo nchi nzima na baadhi ya nchi! 
Jibu la maswali yako yoote wasiliana nasi:-
Magomeni Mapipa 
 +255789476655/659161111/714973797.
Email:mustaphamadish@gmail.com

 linapotokea la kuchekesha
Share:

Oct 20, 2013

OFFICE INSTALLATIONS

+255789476655/659161111
Hapa ilitakiwa lifungwe Dish moja isipokuwa liende kwenye tv zipatazo nne,na kila mmoja awe anachange channel kupitia Remote yake kwa channel aipendayo bila kumghasi mwengine!
Kuna njia mbili:
1.Kuchagua Channel muhimu tu kama tunavyofanya kwenye Hotel.
2.Kufunga kila mmoja na Receiver/Decoder yake na burudani kama kawa.
Hapa walipendelea kila tv iwe na Decoder yake na walichohitaji ni Dstv tu,hivyo haikuwa issue mi nikafuata nilichopaswa kufanya,nikapiga a/c mbili extra view decoder nne na dish 1 ikawa pouwah!!





Dish na lnb ya njia nne

Flat screen na Extra view

Flat screen na Extra view
Hivyo nikafunga na Flat screen pamoja na Projector mambo yakawa kama nilivyotumwa!
Kazi safi,nzuri na ya kupendeza!
Share:

Oct 18, 2013

AZSKY

Leo nimeonelea niongelee kwa uchache kuhusu hii Receiver kutokana na ukweli kwamba naulizwa sana kuhusu hii kitu,wengine wanataka kujua ni kifaa gani na kazi yake,wengine wanataka kujua zinapatikana wapi,wengine wanataka kujua uhalali wake na wengine wanataka kujua uhakika wa hizi Receiver na nyengine zinazofanana na hizi!!
More info nawaletea soon!!!
Share:

Oct 4, 2013

CHANNEL ZA BURE!!!!!!

Kuna kitu watu wengi wanashindwa kuelewa ni kwanini Aljazeera na Abudhab malipo yao ni rahisi pengine tofauti na Dstv hivi!! Ukweli ni kwamba hawa jamaa wana channel chache sana na ni za sport tu isipokuwa Satellite ambayo wanatumia kuna channel nyingi za bure hivyo humpumbaza mteja na kuona wanachannel nyingi malipo yao kidogo!!
 Ambacho nataka kukwambia ukitumia Receiver ya kwaida na ukaelekeza Dish yako NILESAT unakamata channel kibao za bure!!
Nilesat ama kwa waliozoea ukiwaambia Aljazeera,unaweza ukakamata kwa kutumia Dish zifuatazo:-

KU ft 4

KU ft4 ikitimizwa!

C band ft6 tayari kwa kuweka KU lnb

C band ft6 imekamilika

 Pia unaweza ukapata kwa kutumia C band ft8!!!

Share:

Oct 1, 2013

TRENET KWENYE DISH NAYO!!

Digital ndo habari ya sasa!
Sasa ile channel ya dini ya Trenet tv nayo kwenye Dish tena ikiwa bure!
Unaipata kutumia Dish ndogo,satellite husika Intelsat 17 nyuzi 66E,kama muelewa wa masuala ya madish tofauti nyuzi mbili na Emanuel tv kwenye dish ya KU!!!
Kwa mtazamo wangu wanaweza wakaja kuhama Satellite baadae maana hapa walipokaa wapo wenyewe tu kwa Tanzania hivyo wanaweza wakahamia zilipo nyengine ili kuwapa urahisi wapenzi wa channel hiyo ila kama wataendelea kuka hapo hapo inaweza ikawa mtihani kidogo kwa wadau!!
Share:

Sep 29, 2013

HATIMAE CLOUDS TV KWENYE DISH!!


Swali la wengi leo limepata jibu maana walikuwa wanauliza Clouds tv mbona haipo kwenye Dish,ukweli ni kwamba hili lilikuwa ni swala lililo ndani ya uwezo wa Clouds Media Group na sio mimi Mustapha Madish!!
wamefanya walichopaswa kufanya,ambapo kwangu imekuwa fulsa ndo hivi naitumia kuwaunganisha watu kuangalia clouds tv kupitia Dish,uzuri wake ni kwenye Dish ndogo pale pale zinapopatika zile za Local!!!
Hii inafanya idadi ya channel za Tanzania zinazopatikana kwenye Dish ndogo kuongezeka!!
Zaidi ya yote unapaswa utumie Receiver ya MPEG4 na si MPEG2!
Share:

Sep 13, 2013

KAZI NZURI KWA MACHO YAONEKANA!

Awali hapa fundi alipita na kutumia uwezo wake kufanya alichofanya na kuondoka,lakini haikupita muda kwa mujibu wa mwenyewe Dish ikazingua na fundi akipigiwa kimyaaaa!!
Wapi alipo MustaphaMadish baada ya kunipata solution ikapatikana!!
Kwanza labda nitoe angalizo kwa wateja na mafundi wote kama mimi Dish iliikae muda mwingi bila kusumbua ni lazima ikae sehemu ambayo unaweza kudril,vinginevyo itakuwa kila siku fundi hachezi mbali nawe!!
Hapa nilikuta Dish imewekewa mawe hivyo ikawa kila muda inacheza na kwa kuongezea mawe huchangia Dish kupata kutu maana mvua inaponyesha mawe hunyonya majina mpaka kukauka inachukua muda!

 Toboa toboa inaanza!

 Baada ya toboa!

 Somo linaeleweka!

Toboa inaendelea!

Wakujiita Kenya akikaza kaza!


+255789476655

Share:

Sep 3, 2013

TOKA AFRICANA KWENDA SALASALA

+255789476655/659161111/714973797
Ukija kwenye swala la kuhama toka nyumba moja mpaka nyengineni ni jambo la kawaida sana kuhama na Dish yako iwe ya DSTV ama ya kawaida yeyote ile unahama nayo na channel zako zile zile ama zinaweza kuzidi kama ulikuwa hujui!!!!
Ambacho wengi hawajui na kuona ni kitu cha kawaida tu kuifungua Dish iliyokwishafungwa then unatafuta fundi wakati wa kutaka kufunga ulihamia je unajua madhara ya kuifungua mwenyewe ikiwa haupo makini!!??
Kwanza unaweza ukaiharibu LNB!
Unaweza ukalipinda Dish na kumpa shida fundi wakati wa kufunga!
Hii inatokea kwenye ufunguaji na ubebaji pia toka ulipohama mpaka ulipohamia!
Lakini kama utaifungua kwa umakini inawezaekana kila kitu kikafika salama.
Hii ni DSTV ilikuwa naitoa Mbezi Africana na kwenda kuifunga Mbezi salasala kama ambavyo mwenyeji wangu alivyonituma!

 Hapa nafanya setting zangu

Hapa tayari signal za kumwaga  ila haijalipiwa
Share:

Sep 1, 2013

CHANNEL ZA TANZANIA KWENYE DISH NDOGO


Awali ilikuwa huwezi kupata Local channel mpaka ufunge dish ya c band yaani dish kubwa,lakini sasa mambo ni tofauti kwani unaweza kupata Local channel kwa kutumia kadish kadogo (KU) na lnb ya ku,isipokuwa Receiver ni lazima utumie ya MPEG4 tofauti na upatikanaji wa kwenye c band ambapo hata kwa MPEG2 unapata Local channel!
Channel za Tanzania zainazopatikana kwenye Dish ndogo:-
  1. TBC
  2. CAPITAL
  3. EATV
  4. ITV
  5. CHANNEL 10
  6. ATN
  7. STAR TV 
na nyenginezo za nje ikiwemo Emanuel tv kwa wale wapenzi wa Gospel!
+255789476655/714973797
Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita