Call / WhatsApp +255673378129

Nov 2, 2013

HOTEL INSTALLATIONS

Kwanza ujue unachohitaji!
Channel gani na ngapi,je za kulipia ama za bure,vinginevyo iwe mchanganyiko za bure na kulipia!
Vyote ukishindwa utapata nafasi ya kupatiwa ushauri kwa zile channel pendwa na maelewano yatakapopita kazi ndipo inaanza kama furaha itawale kwako!
Ili uimara upatikane!
 Macho hayana pazia!
Matunda yangu akiwajibika!


 Hotel inapendeza na Flat Screen!
 ...........!!
Receivers

 Vimehusika!

 Vihusishi!

 Hotel tayari kwa kupokea wateja!
Installations hii inaweza kufanyika katika Lodge,Hotel na Guest House!
Kila tv inajitegemea katika kubadili channel bila kumbugudhi mwengine!
+255789476655/659161111

Share:

Nov 1, 2013

KUTOKA KWA MUSTAPHA MADISH

Mustapha MaDish
Si kwamba najua kila kitu ila najua vitu vingi ukanda huu na nashukuru Mungu kupitia hii blog yangu nimeweza kupata kazi nyingi na kujuana na mafundi wenzangu wengi tu Tanzania na nje ya Tanzania na ushirikiano mzuri uliopo ndo uliopelekea mi kuwepo hapa hii leo.
Ni ukweli ulio wazi hii ndo blog ya kwanza Tanzania kama sio East Africa kwa ujumla kuanzishwa inayohusiana na mambo haya hususani kwa lugha yetu ya kiswahili!
Sina muda mrefu sana toka nianze kazi hii ila nina experience ya kutosha sana maana mwezi wa 12/2013 nafikisha mwaka wa saba (7) nikiwa fundi Madish na vyote vinavyohusiana!
Katika kazi za zamani nakumbuka enzi ya GTV na mteja mmoja kati ya wengi ninayemkumbuka kumfungia ni Mh.John Cheyo nyumbani kwake Masaki jijini Dar!
Kazi hii nimesababisha vijana wenzangu wapatao 9 nao waishi kupitia kazi hii yaani nimewafundisha na sasa mafundi wa kutegemewa na wengine wamepata ajira DSTV!

 Matiko

 Kenya
Baadhi ya ninaojivunia na watakuja kuwa moto zaidi ya Mustapha MaDish!
Ijapokuwa wapo ambao mpaka leo nikiwaambia kuwa mimi sijui kila kitu hawaamini ingawaje toka nianze kazi sijawahi kushindwa na kazi isipokuwa napata changamoto tu!
Blog imenifanya niwafikie watu wengi duniani kwa muda mchache na ntaendelea kushukuru kwa ushirikiano wenu wadau!
Ambacho kinanisikitisha kuna watu hawapo serious kabisa na juhudi za mtu,hivyo kwa kutumia no.zangu nilizotoa hapo mtu anakazana kukubeep,wakati mwengine unampigia cha maana hana anachoongea ama anakuuliza kuhusu mambo ya madish,ni sawa sababu ni kazi yangu ila ntawapigia wangapi wasioeleweka!!? pia wakati mwengine mtu unamsaidia pengine frequency hakuamini anaomba no.ya fundi mwengine matokeo yake yule fundi mwengine anarejea tena kwangu na kutaka msaada!
Mimi sifanyi kazi ya kubahatisha kwamaana najua ambacho nafanya na kama ntakwambia kitu fulani hakiwezekani jua hakiwezekani sababu simjibu mtu ambacho sikijui na mpakanakujibu nimeshafanya utafiti!
Ushirikiano ninaoutoa kwa mafundi wenzangu na wadau kiushauri ama frequency sihitaji malipo na sijawahi kumtoza mtu pesa ingawaje mara nyingi watu wanataka kufanya hivyo ukisema tu Ahsante kwangu ni malipo tosha!
Malipo unayopaswa kunilipa ni kunitoa nilipo na kuja kukufanyia kazi na si vinginevyo,mwisho wa yote kutoa frequency ama ushauri wowote kwa mafundi ama wadau wengine si lazima maana kuna watu wengine huwa wananikwaza sana kanakwamba nipo kwa ajili yake yeye tu yaani hata kama nna kazi niache ili nimtajie yeye frequency fulani inakuwa haupo sahihi ndugu zangu tuwe wastaarabu!
Nawashukuru sana!
Toka kwangu .
 Mustapha Hanya.
Share:

TING WAMEHAMA SATELLITE


Niliwahi kuwaambia baadhi ya watu ila ikawa kama hawanielewi hivi baada ya kukataa kuwafungia local channels kupitia Dish dogo baada kugundua kama hizo local uhai wake mdogo,kwa maana satellite waliyokuwa wamewekwa na Ting kwa lugha nyepesi ilikuwa ni mali ya Ting!!
Awali Ting walikuwa Eutelsat 36A degree 36.0E,ambapo walikuwa sawa na Dstv wale wadau watakuwa wanakumbuka kwakuwa ilikuwa unaweza ukatumia Dish moja kwa kupata Ting na Dstv!!
Sasa wamehamia Amos 5 degree 17.0E wala sio mbali saaana na ilipokuwa awali!
Kama wewe ni fundi haya!
Satellite: Amos 5 - 17 degrees East
Frequency: 12417Mhz
Symbol Rate: 30000Msps
Modulation: 8 PSK
FEC : 2/3
Pilots On
Share:

Oct 23, 2013

AZAM TV

Mustapha MaDish  nikiwa Azam tv HQ
Niseme tu ukweli katika ujio wa ving'amuzi vyote Tanzania huu ni ujio tofauti sana,kwa maana kabla ya kuanza kuuza wadau wamekuwa na shauku ya kutaka kununua bila kujua nini kilichopo ila tu wanaamini itakuwa king'amuzi bora kuliko ving'amuzi vyote vilivyopo Tanzania ukiweka mbali wakongwe Dstv,sababu kubwa ikiwa ni mmiliki wa hii kampuni kwa kuwa muda mrefu katika biashara si ya ving'amuzi ila biashara nyengine na sifa yake kuu bidhaa bora kwa bei nafuu,hivyo imani ya watanzania ni kwamba unafuu unakuja!!
Swali je Azam tv ni bei rahisi kweli ama magumashi!!??
VIFAA NI TSH 135000/= BILA UFUNDI
Kujua vifurushi Bofya Hapa
Mustapha MaDish kwa site!

Hapa milele

 Mkataba

 Burudani kwa wote

 Sehemu sahihi ya wewe kuhudumiwa

 Mwendo ule ule

 Mustapha MaDish ameshafanya yake
Niseme tu ukweli katika ujio wa ving'amuzi vyote Tanzania huu ni ujio tofauti sana,kwa maana hawajaanza kuuza isipokuwa wadau wamekuwa na shauku ya kutaka kununua bila kujua nini kilichopo ila tu wanaamini itakuwa king'amuzi bora kuliko ving'amuzi vyote vilivyopo Tanzania ukiweka mbali wakongwe Dstv,sababu kubwa ikiwa ni mmiliki wa hii kampuni kwa kuwa muda mrefu katika biashara si ya ving'amuzi ila biashara nyengine na sifa yake kuu bidhaa bora kwa bei nafuu!!
Swali je Azam tv ni bei rahisi kweli ama magumashi!!??
Bei ni Tsh.135000/= Unapata Dish,Decoder.lnb,Cable 
hii inakuwa haina kufungiwa na kufungiwa ni tsh 30,000/=
Baada ya hapo unachagua vifurushi ili upate vifurushi Bofya Hapa

  Haya kazi ni kwako je ni rahisi ama ghari!!??
Ila mi nilichopenda kutumia Dish tofauti na baadhi ya ving'amuzi vyengine wanaotumia Antenna hii inamaanisha watakuwepo nchi nzima na baadhi ya nchi! 
Jibu la maswali yako yoote wasiliana nasi:-
Magomeni Mapipa 
 +255789476655/659161111/714973797.
Email:mustaphamadish@gmail.com

 linapotokea la kuchekesha
Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita