Call / WhatsApp +255673378129

Dec 7, 2014

GRAND CONFECTIONARY BAKERY LTD | ZUKU INSTALLATION


Hapa ni maeneo ya Keko Mwanga jengo la pili toka Lab Equipment,nazungumzia Bakery ya Grand Confectinary wala si la kujiuliza walitupataje ama kwanini tumefika hapa!
Mwendo ni ule ule wa kupiga no.+255789476655 unachagua king'amuzi utakacho,unasema ulipo kisha sisi tunakufata ulipo,unafungiwa na kulipa papo hapo!


Kwakuwa kazi safi ndo jadi yetu,kwanini usimwambie umpendae kama hii ndo nyumba ya ving'amuzi,gharama zetu ni za kawaida sana ambazo kila mtanzania anaweza kumudu!

MUSTAPHA MADISH | +255789476655
Share:

Dec 6, 2014

AIRTEL DIGITAL TV | KING'AMUZI CHA AIRTEL


La kwanza ambalo utajiuliza  mitandao ya simu nayo inachangamkia fursa!?
Ikumbukwe ya kuwa mwaka ndio mwaka wa mwisho kutumia Analogue,ifikapo tarehe 31 mwezi huu,saa 23:59 tunachotakiwa labda kuizungumzia Analogue tu lakini si kudeal nayo...
Lakini ambapo tunaelekea kuisahau kabisa Analogue leo hii mtu ukimuuliza ni nini maana ya Digital hajui na mwengine anajua ni King'amuzi tu kamaliza...
Kuingia mfumo wa Digital pekee bila kuhusisha Analogue ndipo imetulazimu kutumia Ving'amuzi na sababu hii ndio iliyopelekea kukawa na ving'amuzi kibao vipya achilia mbali vile vikongwe..
Airtel Digital Tv..
Hiki nacho ni king'amuzi kama ilivyo ving'amuzi vyengine vya kulipia..
Inatumia Satellite ya SES-7  Nyuzi 108.2E
Ina channels 383 ambapo za HD ni 25
Decoder yake inauwezo wa kurekodi masaa 150
Ijapokuwa mtandao wa Airtel upo hapa kwetu Tanzania lakini king'amuzi hiki kinatumia India tu kwa sasa,sina lolote la kuzungumza kama je na Tanzania kitakuja king'amuzi hiki..
Kwa maelezo zaidi kuhusu king'amuzi hiki Bofya Hapa


+255789476655 | MUSTAPHA MADISH
Share:

Dec 2, 2014

DCB HQ| DIGITEK INSTALLATION


Hapa ilikwisha fungwa Digitek muda tu ila kutokana na ujenzi wa kupanisha ghorofa mbili zaidi iliwalazimu kuitoa Antenna ilipofungwa awali na kungoja mpaka ujenzi umalizike ili itafutwe pa kufunga tena ili burudani iendelee kama ilivyo awali!
Safari hii wala sikuiweka juu kabisa kama ilivyo awali,tukafanya ya kufanya wazungu wa Digitek wakarudi kisha tukachapa mwendo!

INSTALLATION OF TV SYSTEM | IN OFFICE | IN HOTEL | +255789476655
Share:

Dec 1, 2014

ITV KWENYE DSTV

Ni mapenzi ya wateja wengi wa DStv pindi watakapoona ITV ikiwa inapatikana kwenye king'amuzi hicho na hii pia itapelekea kuwashawishi wengine ili waweze kujiunga na familia ya DStv!
ITV ni miongoni mwa channel za Tanzania zinazopendwa sana licha ya vipindi vyake na kwa habari pia,hii ndo sababu iliyopelekea kuwa na wapenzi wengi sana ndani na nje ya Tanzania.
IMESHAINGIA BOFYA NO.293!
Ili uweze kuona ni rahisi sana kama tayari umeshakuwa mteja wa DStv bofya no.293 ila kama bado hujawa mwana familia wa DStv hujachelewa piga no.+255789476655 ili upate njia rahisi ya kuwa mwanafamilia wa DStv ukiwa hapo hapo ulipo tunakufata!
Kwa mujibu wa wadau wangu DStv itakuwa imebakisha channel moja tu muhimu ambayo ni Clouds tv,hivyo kama nayo itapatikana kiu ya wadau itakuwa imekata!


HUDUMA ZOTE ZA DSTV | TUNAKUFATA ULIPO TUNAKUUNGANISHA | 0789476655
Share:

ZUKU PACKAGES | VIFURUSHI VYA ZUKU


Lengo la kuwa na vifurushi tofauti ni kutoa fulsa kwa kila mdau kuweza kununua na kufanya malipo ya mwezi kutokana na uwezo wake.
Hivi ndivyo vifurushi vya Zuku,idadi ya channel na bei kwa ujumla:-

KUPATA BEI NA VIFURUSHI VIPYA VYA ZUKU TV BOFYA HAPA
1-ZUKU SMART PACKAGE
Ina channel 30 safi.
Malipo Tsh 10,000
Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!

2-ZUKU CLASSIC PACKAGE
Ina channel 69 safi.
Malipo ni Tsh 18,000
Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!

3-ZUKU PREMIUM PACKAGE
Ina channel 100 safi.
Malipo ni Tsh 25,000
Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!

4-ZUKU ASIA PACKAGE
Ina channel 27 safi.
Malipo ni Tsh 24,000
Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!

RADIO
Ina channel 50 safi.
Bofya Hapa kujua Radio zilizopo!

+255 789 476 655
Share:

Nov 26, 2014

MIEZI MITATU BURE | TOKA KWANGU | KUJA KWAKO


Cha kwanza unachojiuliza ni miezi mitatu ya bure toka kwangu kuja kwako ni ya nini!?....
Nagawa ving'amuzi....?
Nawalipia Malipo ya mwezi.......??
Nafunga ving'amuzi bure.......??
Jibu lake ni rahisi sana....!!


1.Chukua simu yako bofya no.+255789476655
2.Chagua king'amuzi ukipendacho
au sema channel upendazo ili upate ushauri king'amuzi gani sahihi kwako.
3.Tayari una king'amuzi ila una tatizo la signal,picha inakatakata.
4.Unataka kuhama na king'amuzi chako?
5.Umenunua king'amuzi chochote popote na unahitaji kufungiwa?

MIEZI MITATU
Ikiwa tutakufungia king'amuzi chochote..
Iwe kipya,umenunua kwetu ama laa!
Iwe cha zamani ila tumekuja kukurekebishia!
Iwe tumekuhamisha toka sehemu moja kwenda nyengine!
Utapata huduma bure ndani ya miezi mitatu baada ya kukufungia/kukurekebishia kwa mara ya kwanza.
Hii ni kwa wateja wote kuanzia tarehe 01/12/2014
Hii inatokana na kujua ambacho nakifanya na kuwa na uhakika nacho ijapokuwa hata makampuni mengine ya ving'amuzi wanatoa miezi mitatu baada ya hapo unalipa pesa kila fundi anapokuja..
Kwanini ulipe mara kwa mara kwa fundi wako?
Lipa mara moja pata huduma miezi mitatu bure!
Ila hii ni kwa ving'amuzi vyote vinavyotumia Dish!
Iwe DSTV,ZUKU TV,AZAM TV,STARTIMES,CONTINENTAL
Ntabaki kuwa mbora na wengine watafata daima milele!
Ulipo nipo nawe piga sasa +255789476655
mustaphamadish@gmail.com
Share:

Nov 23, 2014

OFFER YA STARTIMES TSH 59000/=


Tarehe 24/11/2014 rasmi offer inaanza kwa wateja wote wapya!
Hii inakuwa inajumuisha na malipo ya mwezi mmoja!
Swai ambalo ungetamani kuniuliza ni je Startimes hiyo ni ya Dish ama Antenna!
Jibu ni kwamba hii ni offer kwa Startimes ya Antenna!
Wakati ni wako kuchangamkia hii offer

YOTE KUHUSU STARTIMES | PIGA +255789476655
Share:

Nov 19, 2014

OFFER YA DSTV EXPLORA


Hii maana yake Multichoice Tanzania ( DStv ) imekusudia kila mtu apate kilicho bora kwa bei nafuu na kwa wakati !
Kwa sasa ili umiliki Decoder ya Explora sio lazima mfuko wako uwe umetuuuna la!
Kwa Tsh 281,000 tu unapata Decoder yako ya Explora!
Unazijua sifa za Explora wewe!?



PIGA SIMU +255789476655 | YOTE KUHUSU DSTV
Share:

Nov 14, 2014

AZAM TV | UBUNGO FLAT

Hapa bada niwe tu mkweli,awali nilikuja kufunga Continental ya Dish ila mteja wangu huyu alinunua mwenyewe Decoder ambapo dish alikuwa nayo nilichofanya ni kufanya yangu ili Channel za Continental ziweze kumwagika bila chenga!
Yap nikafanya ya kufanya zikajaa ambapo idadi ikafika kama 90 hivi zote zikiwa buree!!
Ila kilichotokea ndicho kilichopelkekea huyu mteja kuuliza king'amuzi kingine na ndipo akaangukia kwenye hii Azam tv....!!

Mashine ikipambana na zege..

Nguvu kidogo...

Hapa mteja atanisahau!

Sababu ya kuwa tofauti na wengine..

...............!!



Baada ya hapo unadhani ntamalizaje kama si kama hivi:-
KUPATA AZAM TV | PIGA +255789476655 | TUNAKULETEA ULIPO.
Share:

UNAIJUA CABLE TV !?


Maswali yamekuwa meengi mkitaka kujua cable tv inafanyaje kazi na huku wengine mkitaka kujua namna ya kuanzisha cable tv zenu huku mkitoa ushuhuda jinsi zilivyo na wapenzi hasa mikoani kwakuwa ni rahisi sana tofauti na huduma nyengine za ving'amuzi...!!
Je kweli ni rahisi!?
Je unaweza ukaanzisha cable tv yako??
Unajua cable tv ni nini?
Nipo hapa kukujuza yote yanayohusu mambo ya tv channels,hivyo ni jukumu lako kuuliza na hata kutoa maoni yako...
Nitazungumzia CABLE TV kinagaubaga lakini naomba iwe ahadi isiwe leo,ambacho unapaswa kufanya ni kufatana nami ili usipitwe na kapost hicho hiyo siku ikifika!
JIFUNZE KUHUSU VING'AMUZI | PATA HABARI | PATA HUDUMA BORA

Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita