Call / WhatsApp +255673378129

Jun 19, 2015

RAMADHANI KAREEM


Tumeanza mwezi,mwezi ambao kwetu sisi waislamu una maana kubwa sana kwa haraka haraka tu huu ndio mwezi ambao quraan tukufu ndio ilishushwa mwezi huu na kwa uchache zaidi ndio mwezi ambao mwenyezi mungu anatusamehe dhambi zetu tulizonazo na tutakazokuwa nazo,ni mwezi ambao sio ombi bali ni lazima kwa kila aliyejaaliwa kufunga maana yake ni kwamba kama huna tatizo lolote kiafya litakalokufanya ushindwe kufunga ni lazima kufunga..
Mwezi huu unatukumbusha kuacha yale yote ambayo mwenyezi mungu ametukataza kama kuzini,kusengenya,kuongopa,kuiba,nk pia tunakumbushwa kwa nguvu zote kufanya yale tunayostahili kufanya kwa imani zetu kama kuswali,kutoa sadaka na kwenda hija kwa walio na uwezo..
Tunafundishwa kufunga na kuswali,kufunga bila ya kuswali sawa na hakuna funga..
Kuna mengi ya kufanya ili funga zetu zikubalike ijapokuwa vijana wana misemo yao kuwa swaumu za mjini zina kazi ila ukitia nia unafunga bila wasi na kumuachia mungu ndiye mwenye kujua umefunga ukiwa sahihi ama lakini kwa kuzingatia misingi yote ya funga.
Ugumu wa vijana wengi katika mwezi huu ni kutamani,sio kula laa kwakuwa katika maisha ya kawaida ya watanzania wengi ni swaumu,ila linawashinda la kuatamani kufanya ngono.
Kuona ndoa nyiingi inapofikia kipindi cha kuelekea mwezi mtukufu ni jibu tosha la nini ambacho namaanisha,sasa kwa ninyi msiooa ama kuolewa swaumu kwenu zikoje!!???
Zaidi ya yote funga njema wapendwa mkumbuke kuswali na kutoa swadaka!

Share:

Jun 18, 2015

LOADING...


Nilichogundua karibu ving'amuzi vyote vina mapungufu na hii inatokana na kujisahau,wafanyakazi kufanyakazi bila juhudi binafsi wanafanya ile bora liende mwisho wa mwezi tukinge,pia makampuni yenyewe husika hayajajipanga katika baadhi ya mambo ili kukabiliana na ushindani uliopo.
Kwa kulitambua hilo tunakuja kuwa mfano kwa makampuni yote ya ving'amuzi ili kuleta changamoto kwa makampuni yaliyolala kuweza kuamka na kutoa huduma stahiki kwa wateja wao..
Tunakuja...
Kaa tayari kutupokea..
Share:

Jun 16, 2015

BEI MPYA YA MALIPO YA MWEZI AZAM TV


Burudani kwa wote..
Kwa mujibu wa Azam tv bei za vifurushi zimepanda kutokana na ungezeko la kodi,
hivyo kile kifurushi cha tsh 10,000/= kimekuwa tsh 12,000/=
kifurushi cha 15,000/= kimekuwa tsh 20,000/=
na kifurushi cha 20,000/= kimekuwa tsh 30,000/=
Pia siku za usoni kinakuja kifurushi kipya ambacho kitakuwa na channels za india tu,
hivyo ili uzione channel za india itakulazimu ulipie kifurushi hicho kipya lakini kwa kipindi hiki ni bure mpaka hapo ambapo itatangazwa.
Kujua channel zilizopo Bofya Hapa
Mambo yote ya kiufundi Azam tv piga : +255789476655

Share:

Jun 10, 2015

VIFURUSHI VYA TING | TING PACKAGES


Hivi ndivyo vifurushi vilivyopo na bei zake kwenye king'amuzi cha Ting kwenye Antenna na kwenye Dish!
1.REGULAR PACKAGE
Inachannel 12+ safi
Malipo ni Tsh 11,000/=
Kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!
Package hii ni kwenye Antenna tu!
2.CLASSIC PACKAGE
Ina channel 30+ safi
Malipo ni Tsh 22,000/=
Kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!
Package hii ni kwenye Antennatu!
1A.REGULAR PACKAGE
Ina channel 25+ safi!
Malipo ni Tsh 16,000/=
Kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!
Package hii ni kwenye Dish tu!
2A.CLASSIC PACKAGE
Ina channel 50+ safi!
Malipo ni Tsh 24,000/=
Kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!
Package hii ni kwenye Dish tu!
Kwa maelezo Zaidi piga +255789476655

Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita