Call / WhatsApp +255673378129

Apr 12, 2016

KOPO HALISAIDII CHOCHOTE KWENYE DISH


Leo nimeonelea niongelee hili jambo kwakuwa ukiachilia kuliona sehemu mbali mbali pia nimekuwa nikulizwa kama kuna umuhimu wa wenye ving'amuzi vya madish kuweka makopo?
 Jambo la awali la kuzingatia king'amuzi kiwe cha Dish ama Antenna kina namna ya ufungaji wake kwa kutumia vifaa vyote vilivyomo kwenye set ya king'amuzi hicho,ikitokea kimojawapo umekiacha ndipo unajikuta nafasi ya kile ulichokiacha inachukuliwa na KOPO!
Kutumia KOPO kunatokana na sababu hizi:-
  • Tuanze kiufundi
- Fundi hupaswi kuacha kutumia kitu chochote kati ya ulivyovikuta kwenye set ya Dish kwakuwa vyote vina kazi yake na ni muhimu sana.

Hapa unamshawishi mteja atafute kopo lilipo ili aweze kufunika akiamini atasaidia angalau kuepusha gharama za kuita ita fundi.

Ukifunga hivi ni kipi ambacho kitamshawishi mteja aongezee ufundi wake wa kuweka kopo?
Fikra za watanzania wengi wanaamini wakifunika na kopo husaidia:-
  • Huzuia kunguru kufanya uharibifu
  • Husaidia picha kutokupotea wakati wa mvua
Niseme tu ukweli KOPO halisaidii chochoteikiwa fundi amefanyakazi safi.
Kupotea kwa Picha kwa dish ndogo kipindi cha mvua ni kawaida kutokana na uwezo mdogo ili kuepuka hili inakulazimu kutumia Dish kubwa ama lnb maalum na kuhusu kunguru fundi akifanyakazi yake vema kunguru hata abembee vipi hawezi kufanya uharibifu!
mustaphamadish@gmail.com
Share:

UMELIPIA NA BADO HUPATI PICHA!?


Hili ni janga kubwa karibia kwa wateja wote wa ving'amuzi vya kulipia,unafanya malipo lakini hupati picha kwa wakti ama hupati picha kabisa!
Njia za kufanya ili usipate usumbufu wakati wa kufanya malipo ya mwezi:-
> Kabla ya kufanya malipo hakikisha unajua bei ya kifurushi unachotaka kulipia
> King'amuzi chako umekiwasha kabla hujafanya malipo
> Ikiwa unalipia kifurushi ambacho ni tofauti na cha awali huna budi kupiga simu ama kufata njia zilizoelekezwa ili kubadili kifurushi
> King'amuzi chako kina Signal ya kutosha

Nini ufanye ikiwa umeshalipia na hukufata njia hizo:-
> Washa king'amuzi chako
> Hakikisha kina Signal kwa kuangalia channel ambayo ipo bure ( mf:ya matangazo )
> Piga simu kwenye kampuni husika ya king'amuzi unachotumia ili ufunguliwe ama upewe maelekezo zaidi na ikitokea umekosa msaada namba hii ni msaada kwako +255789476655
mustaphamadish@gmail.com
Share:

Mar 24, 2016

NINI UFANYE KING'AMUZI CHAKO KIKIPOTEZA SIGNAL!!


Ukiona neno NO SIGNAL ama kwa kukurahisishia ukiona hupati picha kwenye King'amuzi chako na unapata ujumbe ambao hauhusiani na malipo ujue kuna tatizo la Signal lakini utathibitisha vipi kujua kama ni kweli tatizo ni Signal.
> Kila King'amuzi kina channel ya/za bure ( hapa simaanishi Local channel ) ambapo hata ikiwa malipo yako ya mwezi yamekata utaendelea kuangalia tu huwa hazikati,hivyo yakupasa uzijue Channels hizo ili unapoona umepata ujumbe huuelewi jaribu kuweka channels hizo uone zitaonyesha!? Ikiwa zitaonyesha maana yake tatizo sio signal,tatizo litakuwa ni malipo na ikiwa hazitaonyesha jibu lake tatizo ni Signal.Nimejaribu kuwajuza njia hii ya kienyeji kutokana na wengiwetu hizi lugha zilizokuja na ndege ni mtihani nami nimegundua hilo hivyo sitawaacha nitaenda nanyi sambamba!

Cha kufanya ukishajiridhisha kuwa tatizo ni Signal:-
  • Angalia Signal Cable ( waya inayotoka kwenye Dish/Antenna ) ipo sawa?
> Hakuna sehemu iliyochunika/kukatika
> Imechomekwa sawa kwenye King'amuzi chako sehemu ya lnb in/Antenna
> Imechomekwa sawa kwenye Dish/Antenna ya hicho king'amuzi
> Signal Cable ( Coaxial Cable ) Ina nyaya mbili ndani ambazo hazipaswi kugusana ( Siku nitawaeleza kazi za hizo nyaya )

Ikiwa umeona kupo sawa huna budi kuwasiliana na fundi wako ikiwa unamkumbuka ama unaweza kuwasiliana na kampuni husika ya king'amuzi ukikosa msaada piga namba hii +255789476655.

Tatizo linaweza likawa ni nini baada ya hatua za awali kuzifata?
> Yaweza kuwa Dish ama Antenna imepoteza muelekeo wake
> Yaweza kuwa kama king'amuzi cha Dish lnb kufa
> Yaweza kuwa AC ya signal kwenye king'amuzi imekufa
Zaidi ya yote ili kupata uhakika wa nini tatizo ni fundi atakapofika sehemu ya tukio!

IKIWA UMEFANYA MALIPO NA HUPATI PICHA Bofya Hapa

mustaphamadish@gmail.com
+255789476655
Share:

Mar 21, 2016

KIFURUSHI CHA AZAM SPORTS HD HAKIPO TENA!


Hili ni mojawapo kati ya maboresho ya kampuni ya Azam Media kupitia king'amuzi chake cha Azam tv..
Awali kulikuwa na vifurushi kama vitano hivi ambapo ni:-
  1. AZAM PURE PACKAGE tsh 12,000/=
  2. AZAM PLUS PACKAGE tsh 20,000/=
  3. AZAM PLAY PACKAGE tsh 25,000/=
  4. AZAM SPORTS HD PACKAGE tsh 15,000/=
  5. AZAM INDIAN PACKAGE tsh 16,000/=
 Kifurushi cha Azam Sports HD kwanza kikatolewa kujitegemea badala yake kikaongezwa kwenye kila kifurushi kati ya vifurushi vitatu na jambo zuri zaidi kikapunguzwa bei na kuwa tsh 3,000/= Hivyo kama Azam Pure Package badala ya kulipa tsh 12,000/= itakulazimu kulipia tsh 15,000/= ambapo utaona na kifurushi cha Azam Sports HD kwa lugha nyepesi kifurushi cha Azam Sports HD hakipo tena!
UKITAKA KUJUA BEI MPYA YA VIFURUSHI VYA AZAM Bofya Hapa

MAFUNDI +255 789 476 655
Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita