Dec 18, 2010

Kuna TV nyingi ambazo zina AV moja ama mbili na mtumiaji akawa ana vya kuchomeka zaidi ya viwili.
Mf: ana DVD,Receiver,Decoder,King'amuzi na Game labda,hapo hapo TV yako ina AV moja ama mbili hivyo itakuwa inakulazimu kuchomoa na kuchomeka kila muda ambao unataka kuangalia kimojawapo kati ya hivyo,ambapo itakuwa usumbufu licha ya hivyo pia ile kuchomoa chomoa kila wakati AV cable ni rahisi kukatika.
Napenda kukujuza ambacho labda ulikuwa hukijui....!!
kuna kitu kinaitwa AV selector kazi yake ni kuunganisha vyote kwa wakati mmoja,nikiwa na maana ya kuwa kama ni DVD,Receiver,Decoder,King'amuzi na hata Game na vyote ukaona bila kuchomoa chomoa...!!


Kazi yako itakuwa ni kubadili kwa kubonyeza AV selector yenyewe kwa namba husika kwani katika kuchomeka kwako kutakuwa na namba kwa kila ambacho utachomeka kama DVD no.1,Receiver no.2 na vilivyobakia kwa mtindo huo huo hivyo itakuwa ukibonyeza namba 1 itaonyesha DVD,namba 2 Receiver na vyote kulingana na jinsi utakavyobadili.
Kuna AV selector ambazo zinatumia remote na zisizotumia,kuna za umeme na zisizotumia umeme,kuna kuanzia njia tatu na kuendelea.

7:39 AM   Posted by Mustapha Hanya with 2 comments

2 Unasemaje..??:

Dlomen said...

cooooooool

Anonymous said...

kuna AV selector aina ngapi kwani!!?

Call +255789476655

  • Text +255759091445

Follow

Search