Call / WhatsApp +255673378129

Jun 26, 2015

AZAM TV BEI MPYA TSH 135,000/= BILA UFUNDI!


Ingawaje mikoani na sehemu nyingi tu bado wanauza bei wanazojua wao ila bei elekezi ni tsh 135,000 tu,hii inakuwa bila kifurushi wala ufundi!
Ili ufungiwe itakulazimu kulipia tsh 30,000 tu,ambao itakulinda kwa muda wa miezi mitatu na ikitokea ikasumbua fundi atakuja kumaliza tatizo bila gharama yeyote.
Bei ya zamani ya offer ilikuwa tsh 99,000/= ambapo sasa haipo tena.
Bei mpya ni Tsh 135000 utapata Dish,Decoder,Cable,n.k
baada ya kununua ili uweze kuona itakulazimu kuchagua na kulipia moja ya vifurushi vifuatavyo:-
1.AZAM PURE PACKAGE
Ina channel 25+ bora
Bei mpya tsh 12,000/=
Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!

2.AZAM PLUS PACKAGE
Ina channel 50+
Bei mpya tsh 20,000/=
Bofya Hapa kujua channel zilizopo katika kifurushi hiki!

3.AZAM PLAY PACKAGE
Ina channel 80+
Bei mpya tsh 25,000/=
Bofya Hapa kujua channel zilizopo katika kifurushi hiki!

4.AZAM SPORTS Add-On 
Ina channel 4 tu.
Bei tsh 15,000/=

5.INDIAN Add-On
Ina channel 15+
Bei tsh 6,000/=

6.INDIAN Bouquet
Ina channel 23+
Bei tsh 16,000/=


ZINGATIA:Muda wa kupiga simu ni kuanzia saa 08:00 asubuhi - 20:00 usiku.
MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA | CHOCHOTE KUHUSU AZAM TV | +255789476655
Share:

Jun 19, 2015

RAMADHANI KAREEM


Tumeanza mwezi,mwezi ambao kwetu sisi waislamu una maana kubwa sana kwa haraka haraka tu huu ndio mwezi ambao quraan tukufu ndio ilishushwa mwezi huu na kwa uchache zaidi ndio mwezi ambao mwenyezi mungu anatusamehe dhambi zetu tulizonazo na tutakazokuwa nazo,ni mwezi ambao sio ombi bali ni lazima kwa kila aliyejaaliwa kufunga maana yake ni kwamba kama huna tatizo lolote kiafya litakalokufanya ushindwe kufunga ni lazima kufunga..
Mwezi huu unatukumbusha kuacha yale yote ambayo mwenyezi mungu ametukataza kama kuzini,kusengenya,kuongopa,kuiba,nk pia tunakumbushwa kwa nguvu zote kufanya yale tunayostahili kufanya kwa imani zetu kama kuswali,kutoa sadaka na kwenda hija kwa walio na uwezo..
Tunafundishwa kufunga na kuswali,kufunga bila ya kuswali sawa na hakuna funga..
Kuna mengi ya kufanya ili funga zetu zikubalike ijapokuwa vijana wana misemo yao kuwa swaumu za mjini zina kazi ila ukitia nia unafunga bila wasi na kumuachia mungu ndiye mwenye kujua umefunga ukiwa sahihi ama lakini kwa kuzingatia misingi yote ya funga.
Ugumu wa vijana wengi katika mwezi huu ni kutamani,sio kula laa kwakuwa katika maisha ya kawaida ya watanzania wengi ni swaumu,ila linawashinda la kuatamani kufanya ngono.
Kuona ndoa nyiingi inapofikia kipindi cha kuelekea mwezi mtukufu ni jibu tosha la nini ambacho namaanisha,sasa kwa ninyi msiooa ama kuolewa swaumu kwenu zikoje!!???
Zaidi ya yote funga njema wapendwa mkumbuke kuswali na kutoa swadaka!

Share:

Jun 18, 2015

LOADING...


Nilichogundua karibu ving'amuzi vyote vina mapungufu na hii inatokana na kujisahau,wafanyakazi kufanyakazi bila juhudi binafsi wanafanya ile bora liende mwisho wa mwezi tukinge,pia makampuni yenyewe husika hayajajipanga katika baadhi ya mambo ili kukabiliana na ushindani uliopo.
Kwa kulitambua hilo tunakuja kuwa mfano kwa makampuni yote ya ving'amuzi ili kuleta changamoto kwa makampuni yaliyolala kuweza kuamka na kutoa huduma stahiki kwa wateja wao..
Tunakuja...
Kaa tayari kutupokea..
Share:

Jun 16, 2015

BEI MPYA YA MALIPO YA MWEZI AZAM TV


Burudani kwa wote..
Kwa mujibu wa Azam tv bei za vifurushi zimepanda kutokana na ungezeko la kodi,
hivyo kile kifurushi cha tsh 10,000/= kimekuwa tsh 12,000/=
kifurushi cha 15,000/= kimekuwa tsh 20,000/=
na kifurushi cha 20,000/= kimekuwa tsh 30,000/=
Pia siku za usoni kinakuja kifurushi kipya ambacho kitakuwa na channels za india tu,
hivyo ili uzione channel za india itakulazimu ulipie kifurushi hicho kipya lakini kwa kipindi hiki ni bure mpaka hapo ambapo itatangazwa.
Kujua channel zilizopo Bofya Hapa
Mambo yote ya kiufundi Azam tv piga : +255789476655

Share:

Jun 10, 2015

VIFURUSHI VYA TING | TING PACKAGES


Hivi ndivyo vifurushi vilivyopo na bei zake kwenye king'amuzi cha Ting kwenye Antenna na kwenye Dish!
1.REGULAR PACKAGE
Inachannel 12+ safi
Malipo ni Tsh 11,000/=
Kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!
Package hii ni kwenye Antenna tu!
2.CLASSIC PACKAGE
Ina channel 30+ safi
Malipo ni Tsh 22,000/=
Kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!
Package hii ni kwenye Antennatu!
1A.REGULAR PACKAGE
Ina channel 25+ safi!
Malipo ni Tsh 16,000/=
Kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!
Package hii ni kwenye Dish tu!
2A.CLASSIC PACKAGE
Ina channel 50+ safi!
Malipo ni Tsh 24,000/=
Kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!
Package hii ni kwenye Dish tu!
Kwa maelezo Zaidi piga +255789476655

Share:

Jun 9, 2015

KUNUNUA KING'AMUZI CHA ZUKU TV TANZANIA

Remote ya Zuku
Ili kutoa fulsa ya kila mtu aweze kununua kinga'amuzi cha Zuku Tv imeonelea kushusha bei,ambapo sasa ili kununua zuku itakulazimu kulipia Tsh 88,000 tu,badala ya Tsh 95,000/= ila hii inakuwa bila ufundi.
Ili ufungiwe itakulazimu kulipia Tsh 30,000 tu,pesa hii itakulinda ndani ya miezi mitatu kwa lolote likitokea fundi atahusika bila gharama yeyote ya ziada.
Baada ya hapo unachagua Kifurushi kati ya vifurushi vifuatavyo,ingawaje kwa mwezi wa kwanza unapata kifurushi bure!

1-ZUKU SMART PACK PACKAGE
Ina channel 36 safi.
Malipo ni Tsh 8,999
kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!

2-ZUKU SMART PLUS PACKAGE
Ina channel 40 safi.
Malipo ni Tsh 13,000
 kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!
3-ZUKU CLASSIC PACKAGE
Ina channel 69 safi.
Malipo ni Tsh 18,000
Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!

4-ZUKU PREMIUM PACKAGE
Ina channel 98 safi.
Malipo ni Tsh 25,000
Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!

5-ZUKU ASIA PACKAGE
Ina channel 26 safi.
Malipo ni Tsh 24,000
Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!
ZINGATIA:Muda wakupiga simu ni saa 08:00 - saa 20:00 usiku.

Ili Kununua | Kupata Mafundi | Msaada 
Piga +255714973797
Share:

May 18, 2015

KWANINI TUMELAZIMIKA KUIGIA DIGITAL NA KUACHANA NA ANALOGUE?


Mabadiliko katika mfumo wa utangazaji kutoka mfumo wa analojia kwenda katika mfumo wa dijitali ni utaratibu ambao unaendelea ulimwenguni kote. Mabadiliko haya yanatokana na makubaliano ya nchi wanachama wa Shirika la Umoja wa Mataifa lenye dhamana ya masuala ya mawasiliano yaani International Telecommucations Union yaliyofanyika mwaka 2005 huko Geneva, Uswisi. Makubaliano ya nchi wanachama ni kuzima kabisa matangazo katika mfumo wa analojia na kutumia mfumo wa utangazaji wa dijitali ifikapo tarehe 17 Juni 2015. 

Ili kuhakikisha mabadiliko haya yanafanyika kwa ufanisi, tija na pia kutoa muda wa kutosha wa kutekeleza mabadiliko haya, mwaka 2005 Serikali ilianza mchakato wa uhamaji kutoka mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda dijitali ambao ulihusisha wadau wote, wakiwemo wamiliki wa vyombo vya habari na vituo vya utangazaji wa televisheni, hatua kwa hatua, hadi kuridhia ratiba nzima ya uzimaji wa mitambo ya analojia. Kwa kifupi mchakato wa uhamaji ulipitia hatua zifuatazo:

Mwaka 2005:   Waraka wa kwanza wa mashauriano (consultative document) kuhusu umuhimu na faida za kuhama kutoka mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda dijitali ulitayarishwa na kusambazwa kwa wadau wote;

Mwaka 2006:   Waraka wa pili wa mashauriano na mapendekezo ya muundo wa leseni kwenye mfumo wa utangazaji wa teknolojia ya dijitali ulitayarishwa na kusambazwa kwa wadau wote;

Mwaka 2007:   Kamati ya kiufundi inayoshughulikia uhamaji kutoka mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda dijitali iliundwa;

Mwaka 2007:   Mkutano mkuu uliojumuisha vituo vyote vya utangazaji nchini ulifanyika Bagamoyo kupitisha maazimio ya mfumo wa leseni za utangazaji utakaotumika kwenye mfumo wa dijitali;

Mwaka 2010:   Kampuni tatu (3) zilipewa leseni za ujenzi wa miundombinu ya utangazaji ya dijitali. Kampuni tatu zilizopewa leseni za kusambaza matangazo ya dijitali ni Agape Associates Limited, Basic Transmission Limited, na Star Media (T) Limited. Kampuni hizo zilipewa leseni baada ya kuthibitisha kuwa zina uwezo wa kujenga miundombinu ya kurushia matangazo katika mfumo wa dijitali;

Mwaka 2010:   Kamati ya Kitaifa ya Kuratibu Mabadiliko ya Utangazaji toka mfumo wa analojia kwenda dijitali iliundwa. Kamati hii hukutana kila baada ya miezi mitatu kutathmini maendeleo ya ubadilishaji wa mfumo wa utangazaji;

Mwaka 2011:   Kampeni ya Kitaifa ya kuelimisha umma kuhusu mabadiliko ya mfumo wa utangazaji ilizinduliwa rasmi na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa Tanzania rasmi nchi nzima mwisho wa kutumia mfumo wa Analogue ni tarehe 31/12/2014 saa 23;59.
Tukahamia mfumo wa Digital,ambao huu wa ving'amuzi tulionao ijapokuwa ilikuwa mwisho ni tarehe 17/06/2015,kuhama mapema ni namna ya kuangalia je kuna changamoto gani na vipi wahusika wanakabiliana nazo.

+255789476655
Share:

May 11, 2015

VING'AMUZI VINAVYOCHUANA | AZAM TV & DSTV | KIPI NI ZAIDI!?


Dstv ni wakongwe hii haina ubishi,ila ukongwe wa dstv haina maana kuwa hakuna king'amuzi ambacho kinaweza kuja na kufanya vizuri zaidi yake,hii inatokana na kwanza kujua mahitaji ya watazamaji kwa ujumla na kuwatimizia kile wanachokihitaji,unafuu wa bei ukizingatiwa.
Azam tv ni king'amuzi kipya kati ya vyote unavyoviona ila ndio king'amuzi kinachokimbizana na wakongwe,kwanini? kwasababu wameangalia watazamaji wanataka nini na kwa unafuu pia..Ingawaje Azam tv haijakidhi mahitaji wa wadau kwa 100% lakini alau wameweza kwa ukubwa.
Wadau wengi ni wapenzi wa mpira hivyo Azam tv wamefanikiwa kwa mpira wa Tanzania na Dstv bado anang'ang'ania ukongwe wake kwa mpira wa nje.
Ving'amuzi hivi vina mapungufu yake na kinachowakera wengi ni haya hapa:-

MAPUNGUFU YA DSTV
-Kubwa linalolalamikiwa na watanzania wengi ni bei kuwa juu,nikimaanisha malipo ya mwezi na hii inachangia na mtindo unaotumika wa kutumia $ badala ya Tsh.
Madhara ya kuwa bei juu kumefanya wadau watafute kila aina ya njia kuona wanapata uhondo wa dstv ila kwa njia isiyo rasmi,na hii inapelekea kupunguza walipaji halali wa malipo ya mwezi.
-Wana local channel,lakini malipo ya mwezi yanapokata hawaziachi zikawa bure.
Hayo ni mapungufu makubwa kwa Dstv.

MAPUNGUFU YA AZAM TV
-System wanayotumia kushindwa kutambua malipo ya mwezi wanayolipia wateja na kufunguka badala yake ukilipia kifurushi ukipendacho mpaka upige simu,hii imekuwa kero kwa wateja wengi wa azam tv,mteja anakaa mpaka wiki mbili na ikitokea hapigi simu unapita mwezi pasi kuona kile kifurushi alicholipia.
-Mawakala na wauzaji wengine wasio mawakala kuuza bei tofauti na bei sahihi.Hii sio tu mikoani ijapokuwa mikoani lawama hizi ni kubwa lakini hata hapa Dar es salaam wapo wanaouza bei juu tofauti na matangazo yalivyo.
-Picha kupotea kipindi cha mvua,king'amuzi ambacho kinaongoza kwa kupotea signal wakati wa mvua ndogo tu,hii ni kero nyengine kubwa kwa wateja wa Azam tv,kitaalamu hii inatokana na signal kuwa chini hivyo ni jukumu la Azam tv kuongeza signal badala ya 60 zifike alau 80 lakini kinachotakiwa mfikishe 100.
Hayo ni mapungufu makubwa kwa Azam tv.
TOFAUTI KUBWA KATI YA DSTV & AZAM TV
Dstv ana huduma zaidi ya moja kama:-
Extra view-Inakuwezesha kuona channel mbili tofauti kwa tv mbili tofauti kwa a/c moja.
Explora-Inakupa fulsa ya kurecodi saa 150 na mengineyo.
Umiliki na utofauti wa channel.
Dstv inaonyesha mpira wa nje na Azam tv mpira wa ndani.

MUSTAPHA MADISH | +255789476655 | mustaphamadish@gmail.com
Share:

May 1, 2015

STAR TV | AZAM TV | PAMOJA SASA

Awali ilikuwa ili kupata Star tv kwenye king'amuzi cha Azam ilikuwa ni fundi na ufundi wetu tu,kwani ilikuwa tunafunga satellite mbili kwa wakati mmoja ila baadae wenye mali yao hapo Satellite ya Amos 5 wakafanya ya kufanya.
Baada ya vuta nikuvute hatimae sasa Star tv imeungana na Azam tv,hivyo jambo hili limepelekea kila mmiliki wa king'amuzi cha Azam alipokee kwa furaha,huku wale ambao walikuwa wanasita kujiunga na Azam kwasababu hakuna Star tv huu ndo wakati wenu labda mseme lengine.

+255789476655 | HUDUMA ZA AZAM TV
Share:

Apr 27, 2015

MVUA NA VING'AMUZI VYETU


Kwa kawaida mvua inapokuwa inanyesha watu wengi nami nikiwa mmojawapo huwa mapenzi yapo kukaa sehemu tulivu kama panaruhusu unaangalia tv,iwe ni movie ama vyovyote vile ijapokuwa mimi mapenzi yangu kuangalia movie...
Ikiwa una king'amuzi chako na unataka kuangalia huku ukipisha mvua ifanye yake kisha uendelee na ratiba zako..King'amuzi nacho kinagoma kutoa picha..Mvua inaponyesha ving'amuzi vinavyotumia dish ndogo huwa vinaelemewa ila inapokata mvua navyo vinaonyesha picha kama kawaida..Unadhani ni kwanini vinaelemewa? Fuatana nami..






Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita