Katika vitu wanavyofail karibia makampuni yote ya ving'amuzi Tanzania ni CUSTOMER CARE ingawaje baadhi ya makampuni wameboresha lakini si kwa kukidhi mahitji ya wote..
Nilichogundua ni kwamba wateja wengi hawapendi kupokelewa na mashine,muda ambao mteja anasikiliza sauti iliyorekodiwa salio lake linaendelea kuliwa matokeo yake mteja anaweza akatumia zaidi ya 5000 na bado hapati nafasi ya kuongea na mhudumu na mara nyingi simu za makampuni za ving'amuzi huwa ni za mezani ( Landline ).
Kampuni moja tu ya king'amuzi Tanzania ambayo simu zake kama utatumia mtandao unaofanana na hizo namba inakuwa bura huliwi shilingi yako,hili ni zuri na makampuni mengine kama wangetumia utaratibu huu ingekuwa ahueni ijapokuwa tatizo la simu ni moja kati ya matatizo makuu!
Ukiachilia utafutaji wa mtoa huduma kuwa wa tabu pia unapompata huyo mtoa huduma anakuhudumia kana kwamba yeye ndiye aliyekupigia bila kujali kwamba wewe ndiye uliyepiga na huna salio la kutosha na ikitokea simu yako ikakatika pasipo kumaliza tatizo lako hata hawasumbuki kukupigia wakiamini lazima utaweka vocha na kuwapigia tu...
Kuna hili nalo mteja anayekuhudumia unamwambia tatizo lako,inaonyesha uelewa wake mdogo shortcut anaona ni kukwambia ubebe king'amuzi chako na kukipeleka katika ofisi zao,ambapo tatizo hilo linaweza likaelekezeka kwenye simu na tatizo likaisha..
Mbaya kupita zote ni hili la namba za Customer Care kutokuwa hewani muda wa kazi tena inaweza ikawa zaidi ya wiki moja hili ni tatizo!
Kwa leo ni hayo tu!
MUSTAPHA HANYA
mustaphamadish@gmail.com
+255 789 476 655