Call / WhatsApp +255673378129

Mar 18, 2016

STARTIMES KIFURUSHI CHAKO KIKIISHA

 

KUNA AINA MBILI YA VING'AMUZI:-
DISH - kinacotumia Dish
ANTENNA - kinachotumia Antenna

Malipo ya mwezi yanapoisha wengi tunajua ya kuwa Local channel zinabaki ni kweli ila sio kwa ving'amuzi vyote!
Kuna namna mbili ya walivyofanya Startimes vipo ving'amuzi ambavyo malipo ya mwezi yakiisha zinabaki local channel na vipo ving'amuzi malipo ya mwezi yakikata local zinakata na kubaki TBC1 na ya matangazo!
Utajuaje kama kipi ni kipi!?
Wakati unataka kununua king'amuzi cha Startimes iwe ya Dish/Antenna muulize anayekuuzia kuwa king'amuzi hicho ni cha aina gani cha kukata local channel ama kubaki!? Usikimbilie unafuu wa bei kwa maana unapopewa bei mbili bei ya chini ndio ambayo malipo yakikata channel hazibaki!
Ukitaka kujua vifurushi vya Startimes Bofya Hapa
Share:

Mar 17, 2016

AZAM TV KIFURUSHI CHAKO KIKIISHA



Nimeonelea niweke hapa ili wateja wote wa Azam tv na wale wanaotaka kujiunga kulifahamu hili..
Awali ilikuwa usipolipia malipo ya mwezi zinabaki Lacal channel kwa muda wa wiki tatu siku 21..
Lakini sasa utaratibu umebadilika,ambapo kama malipo yako ya mwezi yatakata zitabaki channel mbili tu TBC1 na XTRA tofauti na ilivyokuwa awali..
Hii imepokelewa tofauti na mategemeo ya wateja wengi ambao walidhani kadri siku zinavyozidi kwenda nipo unafuu utakuja kupatikana kama Local channel zote kuwa bure hata usipolipia muda wote!
KWAKO IMEKAAJE HII..!!??
Unajua kama kifurushi cha AZAM SPORT HD hakipo!!??
Unataka kujua bei mpya ya vifurushi na maboresho yaliyofanyika!!?? Bofya Hapa

+255 789 476 655
Share:

Mar 10, 2016

CUSTOMER CARE ZA VING'AMUZI TANZANIA


Katika vitu wanavyofail karibia makampuni yote ya ving'amuzi Tanzania ni CUSTOMER CARE ingawaje baadhi ya makampuni wameboresha lakini si kwa kukidhi mahitji ya wote..
Nilichogundua ni kwamba wateja wengi hawapendi kupokelewa na mashine,muda ambao mteja anasikiliza sauti iliyorekodiwa salio lake linaendelea kuliwa matokeo yake mteja anaweza akatumia zaidi ya 5000 na bado hapati nafasi ya kuongea na mhudumu na mara nyingi simu za makampuni za ving'amuzi huwa ni za mezani ( Landline ).
Kampuni moja tu ya king'amuzi Tanzania ambayo simu zake kama utatumia mtandao unaofanana na hizo namba inakuwa bura huliwi shilingi yako,hili ni zuri na makampuni mengine kama wangetumia utaratibu huu ingekuwa ahueni ijapokuwa tatizo la simu ni moja kati ya matatizo makuu!
Ukiachilia utafutaji wa mtoa huduma kuwa wa tabu pia unapompata huyo mtoa huduma anakuhudumia kana kwamba yeye ndiye aliyekupigia bila kujali kwamba wewe ndiye uliyepiga na huna salio la kutosha na ikitokea simu yako ikakatika pasipo kumaliza tatizo lako hata hawasumbuki kukupigia wakiamini lazima utaweka vocha na kuwapigia tu...
Kuna hili nalo mteja anayekuhudumia unamwambia tatizo lako,inaonyesha uelewa wake mdogo shortcut anaona ni kukwambia ubebe king'amuzi chako na kukipeleka katika ofisi zao,ambapo tatizo hilo linaweza likaelekezeka kwenye simu na tatizo likaisha..
Mbaya kupita zote ni hili la namba za Customer Care kutokuwa hewani muda wa kazi tena inaweza ikawa zaidi ya wiki moja hili ni tatizo!
Kwa leo ni hayo tu!

MUSTAPHA HANYA
mustaphamadish@gmail.com
+255 789 476 655
Share:

Mar 9, 2016

KIFURUSHI CHA ZUKU SMART PACK | TSH 8,999


 Habari njema kwa wateja wa zuku na wale wanaotaka kujiunga na zuku tv ni hii hapa:-
Kwa tsh 8,999
Unapata kuona channel za tv 30
Radio 18
+ Local channel

Punde nitawawekea channel zilizopo....!!

Ukitaka kujua vifurushi vingine vya zuku tv BOFYA HAPA
Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita