Call / WhatsApp +255673378129

Jul 22, 2015

HOTEL TV SYSTEM INSTALLATION

TV INSTALLATION
Mapendekezo ni ya mteja kwa maana mmiliki wa hotel/sehemu yeyote husika 
kwamba tv zikae ukutani ama mezani,kazi yetu ni kutoa ushauri kwa jinsi mazingira yalivyo,je muonekano mzuri ni upi tv kukaa mezani ama ukutani? ingawaje mara nyingi tv kukaa ukutani ndo huwa zinapendeza na salama pia.

CHANNELS INSTALLATION
Tunatoa nafasi kwa muhusika kusema channel anazotaka ambazo angependa kuziona zinapatikana,pia tunatoa ushauri kwa channel atakazo kama zimejitosheleza ama kuna umuhimu wa kupunguza ama kuongeza kutokana na uzoefu tulionao tunajua mapenzi ya wateja wengi wa hotel/office n.k. kwa channel zinazopendwa sana!
- Control room
Hapa tunahifadhi channel zote tunazohitaji,kisha tunazisambaza kwenye tv zote zilizopo kwa ubora mmoja nikiwa na maana quality ya picha ni moja kwa tv zote hata zikiwa 100.

- Remote Control
Kwa kila tv iliyopo kwa kila chumba itajitegemea kubadili channel kwa kupitia Remote ya tv husika bila kumbugudhi anayeangalia tv nyengine.

PROJECTOR INSTALLATION
Kama ilikuwa hujui Projector inatengenezwa kwa masaa maalum,nikiwa na maana ya kuwa mathalani projector imetengezwa  itumike kwa masaa matano ( 5 ) yakitimia masaa matano hakuna njia ya kurenew yale masaa kwa lugha nyepesi itakulazimu ununue projector nyengine.Tupo kwa ajili ya kutoa ushauri na kukufungia pia popote panapostahili.

REPAILING
Inapotokea unakutana na ujumbe mmojawapo kati ya hii ifuatayo jua ya kuwa fundi anahitajika,inaweza kuwa kiushauri ama kiufundi zaidi kwa fundi kufika eneo husika.Ila kwa ushauri wa awali angalia cable yako ipo sawa? angalia je connector yako imekaa sawa? kwa upande wa Receiver/Decoder/tv ama kutoka kwenye Dish ama chanzo chochote cha channel!
- Bad Signal
- Signal Weak
- No Signal
- No Channel
- No Program
- No Service
- Searching for Signal

BAADHI YA KAZI ZA HOTEL TULIZOFANYA:-
- Bahari Lodge
- JB Belmont
- Geraffe View Hotel
- Transit Motel

UZOEFU:-
Yapata miaka nane ( 8 ) Mustapha MaDish nimejikita ukanda huu,nafunga Dish Antenna aina zote kwa channel za bure na kulipia,nadeal na receiver/decoder aina zote,nina team kazi yenye vijana wenye uzoefu unaozidi miaka miwili kwenye taaluma ya ufundi.
Nimefundisha vijana wapatao 17 ambao kwa sasa wanaendesha maisha yao kupitia taaluma hii wengine wakiwa wameajiriwa Multichoice Tanzania ( DStv ) na wengine makampuni mengine.
Najua kiundani kuhusu ving'amuzi vyote vilivyopo Tanzania.


UNA SWALI..?
UNAHITAJI HUDUMA..?
MSAADA ZAIDI..!
PIGA SIMU +255 784378129

Share:

Jul 21, 2015

MBUYU TWITE | AZAM TV & DSTV


Baraka za mikono salama,kazi nzuri kwa wengine imefanya nifike kwa huyu jamaa tegemezi la timu ya young African Mbuyu Twite,tumefunga DSTV na AZAM TV pia!


+255789476655
Share:

Jul 18, 2015

UPO FACEBOOK !!!???



Je blog yetu imekusaidia kwa kiasi fulani,kwa kukupatia maelezo kwa wakati na kwa kina kuhusu ving'amuzi bila kuchagua ama je blog yetu imekusaidia kukuwezesha kupata huduma ya kununua na kufungiwa king'amuzi kwa wakati? Ama imekusaidia kupata mafundi wa kukufungia king'amuzi chako kwa ubora stahiki!
Una maoni yeyote ili tu tuweze kufanya vizuri zaidi ama una la kutukosoa pale tulipoteleza!?
Tupo hapa kupokea yote bila kubagua lolote kwetu ni msaada wa kutufikisha tunapofikiri!
Swali langu je upo FACEBOOK !? kama ndivyo Bofaya Hapa kisha like page yetu ili uweze kuwa miongoni mwa wadau wetu watakaopata chochote kipya kuhusu king'amuzi kwa wakati ama pia waweza kutuandikia chochote na tukakifanyia kazi kwa wakati hata kama haitakuwa umepiga simu.

Share:

Jul 15, 2015

KING'AMUZI KITAKACHOONYESHA KOMBE LA KAGAME 2015

Ni kiu ya wapenzi wengi na maswali yakiwa yanazidi kila kukicha ya kuwa ni king'amuzi gani na kifurushi gani kitaonyesha CECAFA 2015 kombe la Kagame.
Wala nisikupotezee muda jibu ni DStv.
Kama utalipia kifurushi cha Compact Plus utaweza kuona hizi mechi kwa raha bila kukosa hata moja ikiwa live bila chenga!
Na hii ndio ratiba ya mechi:-

Date:18-Jul-15
APR vs Shandy
13:30
SS9 / Select 2

Date:18-Jul-15
Yanga vs Gor Mahia
15:55
SS9 / Select 2

Date:19-Jul-15
Adam City vs Malakia
13:30
SS9 / Select 2

Date:19-Jul-15
Azam FC vs KCCA
15:55
SS9 / Select 2

Date:20-Jul-15
Telecom vs Khartoum-N
13:30
SS9E / Select

Date:20-Jul-15
Gor Mahia vs KMKM
15:55
SS9E / Select

Date:21-Jul-15
Shandy vs LLB AFC
13:30
SS9E / Select

Date:21-Jul-15
Hegaan FC vs APR
15:55
SS9E / Select

Date:22-Jul-15
KCCA vs Adam City
13:30
SS9E / Select

Date:22-Jul-15
Telecom vs Yanga
15:55
SS9E / Select

Date:23-Jul-15
Hegaan FC vs Shandy
13:30
SS9E / Select

Date:23-Jul-15
APR vs LLB FC
15:55
SS9E / Select

Date:24-Jul-15
Khartoum-N vs Gor Mahia
13:30
SS9E / Select

Date:24-Jul-15
KMKM vs Yanga
15:55
SS9E / Select

Date:25-Jul-15
KCCA vs Malakia
13:30
SS9 / Select 2

Date:25-Jul-15
Adam City vs Azam
15:55
SS9E / Select 2

Date 26-Jul-15
Gor Mahia vs Telecom
13:30
SS9E / Select 2

Date 26-Jul-15
Yanga vs Khatoum-N
15:55
SS9E / Select 2

Date 28-Jul-15
Q/Final 1 (B1 vs A3)
13:30
SS9E / Select

Date 28-Jul-15
Q/Final 2 (A1 vs Best Qualifier)
15:55
SS9E / Select

29-Jul-15
Q/Final 3 B2 vs C2
13:30
SS9E / Select

29-Jul-15
Q/Final 4 C1 vs A2
15:55
SS9E / Select

31-Jul-15
S/Final 1 (w-qf3 vs w-qf4)
13:30
SS9E / Select

31-Jul-15
S/Final 2 (w-qf1 vs w-qf2)
15:55
SS9E / Select

02-Aug-15
3rd and 4th Play-off
13:30
SS9E / Select

02-Aug-15
Final:
15:55
SS9E / Select

Mechi zote zitaonyeshwa live!

MSAADA +255789476655
ZINGATIA:muda wa kupiga simu ni saa 08:00 asubuhi - saa 20:00 usiku.
Share:

Jul 1, 2015

DSTV IMESHUKA TSH 79,000= BILA UFUNDI!


Kwa wateja wapya hii inawahusu sana,muda ambao mamlaka ya mapato tanzania imepandisha bei ya kodi kwenye $,jambo lililopelekea pia kupanda kwa gharama za malipo ya mwezi ya vifushi vya ving'amuzi vyote.
Kwa kulizingatia hilo Multichoice Tanzania imeonelea ipunguze gharama za kununua king'amuzi,kwa tsh 79,000 tu unapata Vifaa vyote ikiwa kama Dish,Decoder,cable,n.k. bei hii inakuwa haina ufundi wala kifurushi.
Ili ufungiwe itakulazimu kulipia tsh 30,000,pesa hiyo licha ya kufungiwa pia itakulinda kwa muda wa miezi mitatu kama litatokea lolote la kiufundi,fundi atakuja kwako kuangalia tatizo bila malipo yeyote.
Baada ya hapo unachagua vifurushi kati ya vifuatavyo kisha unalipia ili uweze kupata channel zilizo bora kabisa!

1-DSTV BOMBA PACKAGE
Ina channel 65+ bora
Bei mpya ni Tsh 19,950
Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!

2-DSTV FAMILY PACKAGE
Ina channel 70+ bora
Bei mpya ni Tsh 42,900
Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!

3-DSTV COMPACT PACKAGE
Ina channel 85+ bora
Bei mpya ni Tsh 82,250
Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!

4-DSTV COMPACT PLUS PACKAGE
Ina channel 90+ bora
Bei mpya ni Tsh 122,500
Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!

5-DSTV PREMIUM PACKAGE
Ina channel 120+ bora
Bei mpya ni Tsh 184,000
Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!

KAMA UNA TATIZO LA KIUFUNDI AMA HUDUMA KWA WATEJA Bofya hapa

ZINGATIA:Muda wa kupiga simu ni saa 08:00 asubuhi - 20:00 usiku.

PIGA SIMU +255789476655 | mustaphamadish@gmail.com


Share:

Jun 26, 2015

AZAM TV BEI MPYA TSH 135,000/= BILA UFUNDI!


Ingawaje mikoani na sehemu nyingi tu bado wanauza bei wanazojua wao ila bei elekezi ni tsh 135,000 tu,hii inakuwa bila kifurushi wala ufundi!
Ili ufungiwe itakulazimu kulipia tsh 30,000 tu,ambao itakulinda kwa muda wa miezi mitatu na ikitokea ikasumbua fundi atakuja kumaliza tatizo bila gharama yeyote.
Bei ya zamani ya offer ilikuwa tsh 99,000/= ambapo sasa haipo tena.
Bei mpya ni Tsh 135000 utapata Dish,Decoder,Cable,n.k
baada ya kununua ili uweze kuona itakulazimu kuchagua na kulipia moja ya vifurushi vifuatavyo:-
1.AZAM PURE PACKAGE
Ina channel 25+ bora
Bei mpya tsh 12,000/=
Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!

2.AZAM PLUS PACKAGE
Ina channel 50+
Bei mpya tsh 20,000/=
Bofya Hapa kujua channel zilizopo katika kifurushi hiki!

3.AZAM PLAY PACKAGE
Ina channel 80+
Bei mpya tsh 25,000/=
Bofya Hapa kujua channel zilizopo katika kifurushi hiki!

4.AZAM SPORTS Add-On 
Ina channel 4 tu.
Bei tsh 15,000/=

5.INDIAN Add-On
Ina channel 15+
Bei tsh 6,000/=

6.INDIAN Bouquet
Ina channel 23+
Bei tsh 16,000/=


ZINGATIA:Muda wa kupiga simu ni kuanzia saa 08:00 asubuhi - 20:00 usiku.
MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA | CHOCHOTE KUHUSU AZAM TV | +255789476655
Share:

Jun 19, 2015

RAMADHANI KAREEM


Tumeanza mwezi,mwezi ambao kwetu sisi waislamu una maana kubwa sana kwa haraka haraka tu huu ndio mwezi ambao quraan tukufu ndio ilishushwa mwezi huu na kwa uchache zaidi ndio mwezi ambao mwenyezi mungu anatusamehe dhambi zetu tulizonazo na tutakazokuwa nazo,ni mwezi ambao sio ombi bali ni lazima kwa kila aliyejaaliwa kufunga maana yake ni kwamba kama huna tatizo lolote kiafya litakalokufanya ushindwe kufunga ni lazima kufunga..
Mwezi huu unatukumbusha kuacha yale yote ambayo mwenyezi mungu ametukataza kama kuzini,kusengenya,kuongopa,kuiba,nk pia tunakumbushwa kwa nguvu zote kufanya yale tunayostahili kufanya kwa imani zetu kama kuswali,kutoa sadaka na kwenda hija kwa walio na uwezo..
Tunafundishwa kufunga na kuswali,kufunga bila ya kuswali sawa na hakuna funga..
Kuna mengi ya kufanya ili funga zetu zikubalike ijapokuwa vijana wana misemo yao kuwa swaumu za mjini zina kazi ila ukitia nia unafunga bila wasi na kumuachia mungu ndiye mwenye kujua umefunga ukiwa sahihi ama lakini kwa kuzingatia misingi yote ya funga.
Ugumu wa vijana wengi katika mwezi huu ni kutamani,sio kula laa kwakuwa katika maisha ya kawaida ya watanzania wengi ni swaumu,ila linawashinda la kuatamani kufanya ngono.
Kuona ndoa nyiingi inapofikia kipindi cha kuelekea mwezi mtukufu ni jibu tosha la nini ambacho namaanisha,sasa kwa ninyi msiooa ama kuolewa swaumu kwenu zikoje!!???
Zaidi ya yote funga njema wapendwa mkumbuke kuswali na kutoa swadaka!

Share:

Jun 18, 2015

LOADING...


Nilichogundua karibu ving'amuzi vyote vina mapungufu na hii inatokana na kujisahau,wafanyakazi kufanyakazi bila juhudi binafsi wanafanya ile bora liende mwisho wa mwezi tukinge,pia makampuni yenyewe husika hayajajipanga katika baadhi ya mambo ili kukabiliana na ushindani uliopo.
Kwa kulitambua hilo tunakuja kuwa mfano kwa makampuni yote ya ving'amuzi ili kuleta changamoto kwa makampuni yaliyolala kuweza kuamka na kutoa huduma stahiki kwa wateja wao..
Tunakuja...
Kaa tayari kutupokea..
Share:

Jun 16, 2015

BEI MPYA YA MALIPO YA MWEZI AZAM TV


Burudani kwa wote..
Kwa mujibu wa Azam tv bei za vifurushi zimepanda kutokana na ungezeko la kodi,
hivyo kile kifurushi cha tsh 10,000/= kimekuwa tsh 12,000/=
kifurushi cha 15,000/= kimekuwa tsh 20,000/=
na kifurushi cha 20,000/= kimekuwa tsh 30,000/=
Pia siku za usoni kinakuja kifurushi kipya ambacho kitakuwa na channels za india tu,
hivyo ili uzione channel za india itakulazimu ulipie kifurushi hicho kipya lakini kwa kipindi hiki ni bure mpaka hapo ambapo itatangazwa.
Kujua channel zilizopo Bofya Hapa
Mambo yote ya kiufundi Azam tv piga : +255789476655

Share:

Jun 10, 2015

VIFURUSHI VYA TING | TING PACKAGES


Hivi ndivyo vifurushi vilivyopo na bei zake kwenye king'amuzi cha Ting kwenye Antenna na kwenye Dish!
1.REGULAR PACKAGE
Inachannel 12+ safi
Malipo ni Tsh 11,000/=
Kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!
Package hii ni kwenye Antenna tu!
2.CLASSIC PACKAGE
Ina channel 30+ safi
Malipo ni Tsh 22,000/=
Kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!
Package hii ni kwenye Antennatu!
1A.REGULAR PACKAGE
Ina channel 25+ safi!
Malipo ni Tsh 16,000/=
Kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!
Package hii ni kwenye Dish tu!
2A.CLASSIC PACKAGE
Ina channel 50+ safi!
Malipo ni Tsh 24,000/=
Kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!
Package hii ni kwenye Dish tu!
Kwa maelezo Zaidi piga +255789476655

Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita