Imezoeleka kufanyika kwenye Aparment kubwa,ambapo gharama na hata mfumo wake huwa expensive ila leo nikupe siri, mfumo huu unaweza kuwa rahisi na bora kwako hata wewe ambaye unamiliki nyumba ambayo sio apartment kuubwa, hata nyumba ya kawaida ambayo ina wapangaji ama mnaishi wenyewe tu familia na mngependa kutumia Dish moja ama Antenna moja kwa tv zote zilizopo kwenye nyumba yako na kila tv ikiwa na king'amuzi chake, kinachotumika kwa wote ni Dish ama Antenna isipokuwa king'amuzi kila mtu anakuwa na chake na analipia vile apendavyo! tumeifanya rahisi kwako ambapo kwa gharama ndogo itakuwezesha kumudu. Hii ni kwa wamiliki wa nyumba ambao mmekusudia ziwe za biashara kwa maana kupangisha,tumeona msuguano uliopo hivi sasa kwenye majumba mengi pale ambapo tumepata kazi ya kwenda kufunga madish,kuna upishani kati ya mwenye nyumba na mpangaji na mara nyengine hutokea upishani kati ya fundi na mteja wake ambaye ni mpangaji wa hiyo nyumba,upishani hutokea pale ambapo mmoja anapopendekeza dish ifungwe mahali fulani huku fundi akitaka ifungwe mahali fulani mwisho wa ubishani huu mara zote fundi huwa mshindi kwakuwa dish haifungwi tu kama inavyofungwa Antenna ya kawaida,dish inamuelekeo wake maalumu na ni lazima ufatwe.
Technology ambayo inatumika imewarahisishia wenye nyumba na pia,nikupe faida kiuchache:-wapangaji
Faida kubwa anayopata mwenye nyumba ni kuepuka uharibifu wa nyumba yake. Faida nyengine ni jengo ama nyumba kuwa safi ( Muonekano mzuri )
Faida anazopata mpangaji ni kupunguza gharama za kufunga na kurepair king'amuzi.
Dish ambazo zina wateja wengi.
Antenna.
INAFANYAJE KAZI:-
- Inafungwa Dish moja ama mbili zile zinazopendwa kutokana na eneo ulilopo ama utapata ushauri toka kwetu.
- Unaweza ukafunga na Antenna 1 kama kutakuwa na ulazima huo.
- Inaenda Cable kwa kila Point ya Tv kwa nyumba ama jengo lote husika.
- Kila mpangaji/Mkazi wa hiyo nyumba/jengo atakachopaswa kuhamia nacho/kununua ni king'amuzi tu na kuchomeka pasipo kufunga tena Dish/Antenna.
- Kila kwenye tv ( King'amuzi ) ataweza kufurahia matangazo pasipo kumuingilia mwengine.
- Ikitokea kuna repair wahusika wote watahusishwa ama watahusika kwakuwa Dish/Antenna ni moja.
INAWEZEKANAJE?
Tupigie +255789476655 Whatsapp+255784378129
Email:mustaphamadish@gmail.com
Popote Tanzania ukituhitaji tunafika kwa kazi zifatazo:-
- Kufunga mfumo wa TV kwenye Hotel
- Kufunga mfumo wa TV kwenye Apartment
- Kufunga mfumo wa TV kwenye Nyumba binafsi
- Kufunga mfumo wa TV kwenye Office
- Kufunga mfumo wa TV kweny Lodge/Bar n.k
- Kufunga CCTV Cameras kwenye Hotel/Apartment/Office n.k
- Kufunga Electric Fence kwenye Yard/Apartment/Office n.k