Call / WhatsApp +255673378129

Nov 26, 2015

RATIBA YA AZAM TV

Ilikupata ratiba ya king'amuzi chako cha Azam tv:-
Chukua remote yako,bonyeza 1- menu..

2- Digital TV
 

3- Programme Guide 

4- Chagua channel unayotaka kupata ratiba yake ya wiki nzima kama inavyoonekana hapo juu! 
 
5- Ikiwa maelezo hayajaeleweka kwamsaada Zaidi piga +255789476655
Share:

Nov 25, 2015

KUZIMIKA KWA VING'AMUZI BILA TAARIFA KWA WATEJA!

Idadi ya simu ninazopokea kwa takribani wiki tatu mpaka leo hii ni wateja wa baadhi ya ving'amuzi ambavyo vimekata matangazo yao bila taarifa yeyote kwa wateja wao na kitu kibaya zaidi ushirikiano unakuwa sio mzuri kwa mujibu wa wateja wanaonipigia mimi!


Ving'amuzi vilivyokata ni ZUKU tv.
Ijapokuwa ikarejea hewani ila hakukuwa na taarifa yeyote ama kuwataka radhi wateja wao.
TING nao wakapotea hewani mpaka leo hii na mchezo ni ule ule hakukuwa na taarifa wala kuomba radhi kwa kwa nguvu ile wanayotumia kuuza ving'amuzi!

CONTINENTAL pia hawapo hewani!
Ubaya ambao unatokea hapa taarifa na kuwataka radhi wateja hakuna kwa nguvu ile wanayotumia kuuza king'amuzi na kwa bahati mbaya Continental wana nafasi nzuri ya kufikisha ujumbe kwa umma kupitia Startv ama RFA lakini matangazo yanayoendelea ni yale ya kuuza ving'amuzi!
ANGALIZO TOKA KWA MUSTAPHA MADISH:
Tatizo lililopo kwa Continental na Ting ni satellite waliyopo ya Amos 5:-
Jukumu la makampuni waliyopo Satellite hii walitakiwa watoe taarifa kwa wakati kwa wateja wao ili waendelee kuwa na imani nao kwa maana ipo wazi kifundi tunajua Satellite ya Amos 5 haipo tena imepotea hivyo ili Ting na Continental ni lazima wahame Satellite je watahamia Satellite gani hilo wanalijua wahusika.
Yapo matatizo ambayo huwezi kuyazuia kwakuwa najua vema mfumo mzima ulivyo,yapo ya kuepukika na yapo ambayo hayaepukiki,ila kinachopaswa kufanyika ni kutoa taarifa kwa wakati kwa wateja wenu na kwa umma kwa ujumla huku mkiendelea kutatua tatizo kwa wakati,kukaa kimya kwenu ni kupoteza imani kwa wateja wenu,inaonekana mnatoa huduma mbovu na hii inapelekea kufanya maamuzi ya kuamua kununua king'amuzi kingine!
+255789476655
Share:

Nov 19, 2015

UNATAKA KUJUA NINI KUHUSU DIGITAL TV ?



Yapo mengi ambayo siwezi kuyamaliza kwa siku moja na pia siwezi kuyamaliza ikiwa sijajua ambacho wewe ungependa kujua kuhusu ulimwengu huu wa Digital tv na hata ukihitaji kujua yale ya Analogue tv nipo tayari kukujuza kwa kina kabisa!
Ni nini ambacho ungependa kukijua yawezekana kuhusu king'amuzi chochote kati ya vilivyopo Tanzania ama vinavyotumika Tanzania ingawaje ninauzwa nje ya nchi.Hata kama swali halihusiani na ving'amuzi ila tu linahusiana na ulimwengu huu wa Digital tv nnachoweza kusema karibu alau tuwekane sawa.

NIULIZE:
  • Chochote ambacho ungependa kujua ikiwa kutokea kule tulikotoka Analogue tv ama hapa tulipo Digital tv.
  • Jambo lolote la kiufundi ambalo linakutatiza katika ving'amuzi vyote vilivyopo.

Ili na wengine wanufaike na majibu ya maswali yatakayoulizwa naomba muulize kwenye sehemu ya ku comment nami nitajibia hapo ili maswali yasijirudie!
Share:

Nov 16, 2015

DSTV HUDUMA KWA WATEJA NA KUPATA MAFUNDI WA DSTV


Je unatumia DStv? ama unahitaji kujiunga na DSTV? 
Karibu kwa kufata utaratibu huu:-

IKIWA UNATUMIA DSTV:
  • Umelipia na bado hupati channel?
  • Picha inakatakata ama haionyeshi kabisa
  • Unataka kuhama toka nyumba moja kwenda nyengine
  • Unahitaji kuongeza Decoder nyengine ama kubadili
  • Unahitaji ufafanuzi zaidi kuhusu bei mpya za vifurushi
  • Unahitaji kujua chochote kuhusu huduma za DStv
  • Unahitaji Fundi 
  • Msaada wowote wa kiufundi
Dish ya DStv ikiwa kwenye setting!

Fundi akifanya ufundi wake!

Piga simu namba +255658046655 Kwa msaada zaidi! 

UNAHITAJI KUJIUNGA NA DSTV
  • Kujua Bidhaa zote za DStv
  • Kujua bei halisi/Offer ya kununua king'amuzi
  • Kujua bei halisi ya vifurushi Bofya Hapa
  • Kujua bei ya Ufundi
  • Kujua namna ya kuweza kuunganishwa
  • Kupata huduma ya kuletewa ulipo na kulipia baada ya kuletewa
  • Ikiwa umenunua na hujafungiwa ili upate fundi popote ulipo Tanzania
  • Yote yanayohusu DStv

Piga simu namba +255658046655 Kwa msaada zaidi!


Share:

Nov 1, 2015

VIFURUSHI NA CHANEL ZA STARTIMES



Ni moja kati ya makampuni ambayo yanamiliki ving'amuzi aina mbili tofauti kimasafa,nikiwa na maana ya kuwa kuna aina mbili ya Decoder za startimes:
  • StarTimes ya Antenna
  • StarTime ya Dish
Kwa kukurahisishia startimes wakati wanaanza hapa nchini walianza na mfumo wa kutumia Antenna tu,mfumo huu ukawa na lawama nyingi sana katika swala zima la kukatakata kwa picha wakaja kuboresha kwa kuleta na mfumo wa Dish ingawaje hata ule mfumo wa Antenna nao kwa sasa upo vizuri umeboreshwa!

Hivi ndivyo vifurushi vya StarTime:-

KWA KING'AMUZI CHA DISH

1- KIFURUSHI CHA NYOTA
Ina channels 30+ bora!
Bei yake ni Tsh 11,000 Kwa mwezi
Tsh 4,000 Kwa wiki
Tsh 1,100 Kwa siku
Bofya hapa kujua channels zilizopo kwenye kifurushi hiki!

2- KIFURUSHI CHA SMART
Ina channels 60+ bora!
Bei yake ni Tsh 21,000 Kwa mwezi
Tsh 8,000 Kwa wiki
Tsh 2,100 Kwa siku
Bofya hapa kujua channels zilizopo kwenye kifurushi hiki!

3-STARTIMES SPORT PLUS ( Cha ziada )
Ina channels 4+ bora!
Bei yake ni Tsh 14,000
Bofya hapa kujua channels zilizopo kwenye kifurushi hiki!

4- KIFURUSHI CHA SUPER
Ina channels 100+ bora!
Bei yake ni Tsh 36,000 Kwa mwezi
Tsh 12,000 Kwa wiki
Tsh 3,600 Kwa siku
Bofya hapa kujua channels zilizopo kwenye kifurushi hiki!

5- STARTIMES CHINESE PACKAGE
Inajumuisha kifurushi cha Smart
Ina channels 84+ bora!
Bei ni Tsh 43000
Bofya hapa kujua channels zilizopo katika kifurushi hiki!

6-STARTIMES INDIAN PACKAGE 
Sasa inapatikana kama kifurushi cha ziada
Ina channels 8+ bora!
Bei ni Tsh 18000
Bofya hapa kujua channels zilizopo kwenye kifurushi hiki!

KWA KING'AMUZI CHA ANTENNA

1-  KIFURUSHI CHA NYOTA
Ina channels 30+ bora!
Bei yake ni Tsh 9,000 Kwa mwezi
Tsh 3,000 Kwa wiki
Tsh 900 Kwa wiki
Bofya hapa kujua channels zilizopo kwenye kifurushi hiki!

2-  KIFURUSHI CHA MAMBO
Ina channels 60+ bora!
Bei yake ni Tsh 14,000 Kwa mwezi
Tsh 6,000 Kwa wiki
Tsh 1,500 Kwa siku
Bofya hapa kujua channels zilizopo kwenye kifurushi hiki!

3-  KIFURUSHI CHA UHURU
Ina channels 80+ bora!
Bei yake ni Tsh 20,000 Kwa mwezi
Tsh 7,000 Kwa wiki
Tsh 2,500 Kwa siku
Bofya hapa kujua channels zilizopo kwenye kifurushi hiki!




Kwa Maelezo zaidi
Instagram @mustaphamadish
Call / Whatsapp / Text 
+255 658 046 655
Share:

KING'AMUZI GANI BORA TANZANIA!?


Swali ambalo kila kukicha nakutana nalo kutoka kwenu..
Kwa kuanzia nikwambie ving'amuzi vilivyopo Tanzania ili niweze kukwambia kilicho bora..
Azam tv
 Continental
Coconut Digital tv
DStv
Digitek
Easy tv
Startimes
Ting
Zuku tv
Kwa kuanzia nikwambie ving'amuzi vyote vina ubora wake na mapungufu yake,itakapotokea umemiliki king'amuzi kimojawapo kati ya hivyo lazima utatoa sifa na mapungufu pia ila tatizo linakuja pale mapungufu yanapozidi sifa jibu linakuwa hakifai ila kama itatokea sifa zikazidi mapungufu jibu linakuja ndicho king'amuzi bora.
Ili ujue ni king'amuzi gani bora inapaswa kutambua wewe muhitaji vifuatavyo:-
  • Unataka kuangalia nini? ( Unapendelea channel gani )
  • Unataka kuangalia picha katika ubora upi?
  • Uwezo wako kifedha wa kununua king'amuzi na kufanya malipo ya mwezi?
  •  
Ukishajielewa wewe mwenyewe ndipo unapaswa kufanya hili la pili:-
  • Tafuta chaguo lako lilipo ( Unachotaka kuangalia kipo king'amuzi gani )
  • Ubora wa kampuni husika na Product ( Huduma zitolewazo ni katika misingi inayotakiwa )
  • Uliza kwa mtu ama watu wanaojua ( wanaotumia/waliowahi kutumia ) king'amuzi unachohisi kinakufaa ili kujiridhisha kabla ya kununua.N.B:usiulize kwenye kampuni husika kabla hujauliza kwa wanaotumia kwakuwa kama kampuni inayouza hicho king'amuzi hakitakupa jibu sahihi ila watakupa jibu la kibiashara ili ununue.
  • Uliza hapa +255789476655 tunajua ving'amuzi vyote kiundani zaidi,jibu utakalopata hapa lifanyie kazi.
  •  
King'amuzi gani unachopaswa kununua baada ya kuzingatia hayo:-
  • Ambacho kina Products nzuri na imara.
  • Ambacho kinajali wateja  
  • Ambacho matangazo yake hayakatikati kira mara pasipokuwa na taarifa.
  • Ambacho kina channel nzuri na picha safi.
  •  
Kila king'amuzi kinajitahidi kufanya kila wawezalo ili wawe wabora,wingi wa ving'amuzi umesaidia hili hivyo kila leo uboreshaji unafanyika kama unaona king'amuzi unachotumia hawana dalili ya kuboresha huduma zao unangoja nini kuhama!?
Kuna king'amuzi kilikuwa na wateja wengi sana lakini sasa ama kila kukicha idadi ya wateja inapungua,unadhani ni kutokana na nini? huduma mbovu na kutotaka kubadilika,hili makampuni mengine mjifunze laa sivyo kila kukicha watabadilishwa Ma sales Manager
+255 789 476 655 
Share:

Oct 18, 2015

OCTOBER 25 | FANYA KWELI



NAJIVUNIA KUWA MTANZANIA
Popote nitasimama na kujivunia kuwa mtanzania mzawa,najivunia lugha yetu kiswahili najivunia na mengi mazuri yaliyopo nchini mwangu,nchi huru ambayo najisikia kufanya chochote wakati wowote pasi tu kuvunja sheria...
AMANI  IMESABABISHWA NA UPENDO
Ni jambo tunalojivua mpaka leo hii,sababu kubwa ikiwa ni upendo tulionao baina yetu.Daima tujitahidi kuidumisha amani hii tuliyonayo ambayo ni kama ndoto kwa baadhi ya mataifa mengine.
KIZAZI CHA DIGITAL
Kuna kundi kubwa la vijana ambao naweza kusema ni kizazi cha Digital,nikiwa na maana yakuwa ndio wenye chachu kubwa ya kutaka mabadiliko kuliko kizazi cha Analogue..
UNA KADI YA KUPIGIA KURA?
Zimebaki siku chache mnoo! swali langu ni kwamba una kikatio? ama unampigia kampeni tu mgombea unayempenda ila kura humpigii!!? Je umefikisha umri wa kupiga kura ama unabishana tu kuhusu mgombea unayeona anafaa!?
KWANINI UNAMCHAGUA!?
Unayekusudia kumchagua siku ya kupiga kura october 25,umejiuliza ni kwanini unamchagua!? Unamfahamu? Umekula pesa yake? Unaamini atatekeleza kile alichoahidi? Unampenda tu? Ama kwanini!!?
OCTOBER 25 USIFANYE MAKOSA
Kura yako itasababisha kile unachokitarajia kutokea kitokee,unahitaji tutoke hapa tulipo tuelekee hatua nyengine nzuri zaidi? kura yako ndio itakayoleta mabadiliko hayo!
Tukapige kura tuwachague wale viongozi ambao tunaona watatuletea mabadiliko,watakaotuletea maendeleo na sio vinginevyo.
TUKUBALI MATOKEO
Uchaguzi wa mwaka huu ni tofauti na miaka yote kiukweli kabisa,mwaka huu ile hamasa imekuwa kubwa mno naweza kusema kile kizazi cha Digital hakitaki mchecho wanachotaka kuona mambo yanaenda sawa na si ubabaishaji.Kama ambavyo tunatokea wengi kwenye kampeni tunapaswa kutokea wengi kwenye kupiga kura pia.Jambo la kuzingatia ni kwamba tukubaliane na matokeo yatakayotokea kwa zile kura tutakazopiga.
Ili tuweze kuendelea kuilinda amani yetu tuliojaaliwa na Allah.
+255 MUNGU IBARIKI TANZANIA
Share:

Oct 15, 2015

ZUKU TV TANZANIA VIFURUSHI NA BEI MPYA


 Tsh 75000/= Unapata king'amuzi kikiwa na muda wa kuona wa mwezi mmoja.
Inakuwa na vifaa vyote kama:Dish,Decoder,LNB,Cable na stendi.
HII INAKUWA BILA UFUNDI 
Kwa sasa kuna vifurushi vinne tu navyo ni kama ifatavyo:-
  1. ZUKU CLASSIC TSH 15,500 Per Month - Channels 69. Bofya hapa
  2. ZUKU PREMIUM TSH 22,500 Per Month - Channels 100. Bofya hapa
  3. ZUKU ASIAN TSH 24,000 Per Month - Channels 27 Bofya hapa
  4. ZUKU ASIAN ( yenyewe ) TSH 32,000 Per Month - Channels 33 Bofya hapa
Kwa maelezo zaidi ama msaada kiufundi.
+255659161111/789476655
Share:

Oct 13, 2015

MIEZI MITATU BURE | TUKIKUHUDUMIA


Ikitokea umekuwa mteja wetu kwa mara ya kwanza tumekufungia king'amuzi chochote kile kati ya hivi:-
  • DSTV
  • STARTIMES
  • ZUKU TV
  • AZAM TV
  • CONTINENTAL
Tatizo lolote la kiufundi likitokea ndani ya miezi mitatu tutahusika kwa kukuhudumia pasi kulipia malipo ya ziada ikiwa halijasababishwa na mteja.
Ikitokea umetutafuta na tukakuhudumia kwa kufanya repair king'amuzi chako ambacho hujanunua kwetu,pia huduma hii itakuhusu baada ya kumaliza tatizo lako,nikiwa na maana ya kuwa baada ya huduma zetu ndani ya miezi mitatu tatizo likitokea tunakuhudumia bure.
Hii inajumuisha king'amuzi chochote kiwe cha bure ama kulipia,dish ndogo ama kubwa.

+255789476655
Share:

Oct 10, 2015

NUNUA KING'AMUZI UKIWA KWAKO


PIGA SIMU +255789476655
  • Jitambulishe na mahali ulipo.
  • Chagua king'amuzi chochote kwa matakwa yako.
  • Tutakushauri kabla hujanunua king'amuzi ulichokusudia na vyengine kama utapenda.
  • Tutakapofika muafaka unaletewa king'amuzi ulipo.
  • Na fundi anakufungia papohapo kama ukihitaji hivyo.
  • Kisha unafanya malipo ukiwa hapo ulipo baada ya kuletewa na kufungiwa.
 FAIDA ZA KUNUNUA NA KUFUNGIWA NASI:
  • Chochote kikitokea tunahusika asilimia 100
  • Fundi hatoondoka mpaka kuhakikisha umepata picha (umeona channel)
  • Ufundi ndani ya miezi mitatu ni bure baada ya kufungiwa.
  • Tupo kijamaa zaidi,wateja wetu ni ndugu zetu hivyo upo huru kuzungumza.

+255789476655
Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita