Call / WhatsApp +255673378129

Jul 30, 2016

BEI MPYA YA VIFURUSHI VYA ZUKU TV TANZANIA 2016





Kifurushi cha Smart Plus kimeongezeka huku beo zikiwa pungufu kwa baadhi ya vifurushi pia,mabadiliko hayo ni kama ifatavyo:-

1-ZUKU SMART PACK
Ina channel 30 tv safi.
Channel 18 radio.
+ Channel za Tanzana.
Malipo Tsh 8,999 kwa mwezi.
Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!

2-SMART PLUS
Ina channel 40 tv safi.
Channel 18 radio.
+ Channel za Tanzana.
Malipo Tsh 13,000 kwa mwezi.
Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!

3-ZUKU CLASSIC 
Ina channel 69 tv safi.
Channel 55 radio.
+ Channel za Tanzana.
Malipo Tsh 18,000 kwa mwezi.
Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!

4-ZUKU PREMIUM 
Ina channel 98 tv safi.
Channel 55 radio.
+ Channel za Tanzana.
Malipo Tsh 25,000 kwa mwezi.
Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!

5-ZUKU ASIA PACKAGE
Ina channel 26 safi.
Malipo ni Tsh 24,000 kwa mwezi.
Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!

Kununua Zuku tv  Tsh 88,000 bila ufundi!
Ufundi ni Tsh 30,000!
Piga +255 789 476 655


Share:

Jul 1, 2016

KUEPUKA DISH YAKO KUPATA KUTU

Niwe mkweli katika hili usipopata fundi makini uwezekano wa kuepuka hili ni mdogo sana vinginevyo muhusika uwe makini sana na Fundi wako ingawaje mara nyingi muhusika inakuwia vigumu kuona jinsi fundi wako alivyofunga Dish huko juu ya paa!!

Sababu zinazopelekea Dish kupata kutu kwa haraka:-

Sababu zisizoepukika:-

> Ikiwa Dish inafungwa ufukweni.

> Ikiwa Dish ni FAKE.

Sababu zinazoepukika:-

> Kutokuweka vinavyozuia maji kuingia.


Tuone madhara ya kutotumia vinavyozuia maji kuingia ndani na kukosa pa kutokea!
1
Hii ni Stendi ya kubeba Dish,hiki ni kikalio ( Chini ) ambapo kwa kutokufunika juu,imesababisha maji yameingia na kwakuwa hakuna sehemu maalumu ya kutokea maji yanapoingia,yenyewe yakatafuta njia kwa kutafuna kidogo kidogo mpaka kupata njia kama muonavyo!

2
Huu ni mkono wa kushika LNB,upo mfano wa V,mkono huu ni bomba maana yake kati lipo wazi,upande wa mbele inafungwa LNB ambapo inazima maji kuingia na upande wa nyuma kuna ya kukipachika ili kuzuia maji yasiingie kama ilivyoonyeshwa picha namba ( 5 ) kwakuwa yakiingia kinachotokea pale kwenye mkunjo ndipo maji yatajitengenezea njia kama muonavyo hapo juu!
3
Matokeo yake ile V inageuka vipande viwili baada ya kuliwa na kutu!
4
Ufungwaji Dish wa namna hii ndio unaopelekea madhara tuliyoyaona hapo juu kwenye picha ( 1 - 3 ) jinsi maji yalivyosababisha kutu,ambapo kama fundi angetumia vifaa vyote ipasavyo yasingetokea madhara hayo yaliyotokea!
5
Hivi ndivyo unavyopaswa kufunga Dish yako kwa kutumia Plastic cover ili kuzuia maji yasiingia kwenye bomba ya Stend na mkono wa kushika LNB!

Nadhani kwa uchache umeambulia kidogo kwa maelezo zaidi
+255789476655 
NB:Kupiga kuanzia saa 08:30 - 18:00 
Share:

Jun 30, 2016

KUFUNGA DISH NDOGO ( KU DISH INSTALLATION )

Kwakuwa karibu Ving'amuzi vyote Tanzania vinatumia Dish ndogo leo niwape kasomo haka alau mwenye kujaribu na ajaribu atakapopata wasaa!!
Fanya haya ili uweze kufunga Dish ndogo:-

1.Dish Antenna Assembly:
- Unganisha kifaa kimoja kimoja kama karatasi ya maelekezi inavyoonyesha ili kulikamilisha dish lako bila kuacha hata kimoja kwakuwa kila kimoja kina kazi na umuhimu pia.

2.Unganisha stendi yako ya kubeba dish.





3.Angalia sehemu nzuri ya kufunga Dish ili uanze kufunga stendi yako:
- Hakikisha sehemu unayoifunga mbele hakuna miti itakayozuia kupokea signal.
- Sehemu imara itakayoweza kukaa Dish bila kucheza.
- Unashauriwa kuifunga juu ya usawa wa nyuma/jengo ili isipate kuguswa guswa.

4. Funga stendi yako ya dish sehemu ulipoona panafaa.
5. Funga Dish lako kwenye stendi kwa kulielekezea Satellite uliyoikusudia ( Muelekeo wa king'amuzi husika )
6. Unganisha Coaxial cable ( Signal cable ) kwenye king'amuzi chako kwa nyuma sehemu iliyoandikwa LNB IN kisha unganisha kwenye either kwenye Dish sehemu ya LNB ama kama utakuwa na kitafuta signal (Signal  Finder ),kama utatumia Finder lazima uwe na Test cable ( Kipande cha cable ambacho utachomeka toka kwenye finder mpaka kwenye dish ( LNB ) - Nimetoa mfano wa Finder hii kwakuwa ni rahisi kupatikana na hata bei yake ni ya kawaida ila kuna finder nyengine hazihitaji Test cale.
7. Upo tayari kwa kuanza kutafuta signal. Jinsi ya kutafuta signal ntawaletea somo hilo katika post nyengine!
Tuangalie kwenye video hapo chini!



+255 789 476 655
Share:

Jun 16, 2016

UNAANGALIAJE MPIRA BILA KULIPIA/MALIPO NAFUU!


Wadau/Wateja wa ving'amuzi wakubwa ni wapenzi wa mpira hii ilikuwa hata kabla Tanzania haijaingia katika makubaliano ya kati ya zile nchi zilizoachana na mfumo wa Analogue tv na kuingia katika mfumo wa Digital tv..Hii inatokana na wapenzi wa mpira kutaka kupata mpira kwa njia yeyote ile,hivyo imekuwa kama ndo biashara ikiwa ni mdau wa ving'amuzi ili ufanye mauzo mazuri ni lazima ujue namna ya kupata kuonyesha mpira hii imepelekea kina sisi kuchangamkia fulsa kwanza kutafuta njia za kupatikana kwa channels zinazoonyesha mpira bure/kwa bei nafuu kwa udi na uvumba ili kuweza kuuza kwa wahitaji ukiachilia kampuni iliyo na idhini ya kuonyesha mpira Multichoice ( DStv ) ambayo hakuna mdau yeyote wa mpira ambaye halalamikii bei za DStv hususani Packeges za Sports,hii inapelekea kila kukicha kubuniwa njia za kuibia channels za DStv!
Post hii itakamilika hivi karibuni karibu....
Share:

Jun 13, 2016

JINSI YA KUHAMA KIFURUSHI KWENYE KING'AMUZI CHAKO


Pata msaada wa haraka na updates za Visimbuzi instagram @mustaphamadish
Hili ni moja kati ya yale ambayo ni kero kwa watumiaji wa ving'amuzi kutokana na kutokuwa na uelewa wa kutosha na kukosa sehemu ya kupata maelezo ya kina kama hapa!
Swali la kwanza unatumia king'amuzi gani!?
Ving'amuzi vyote vyenye vifurushi ukilipa kifurushi ambacho si kile ulicholipia mwezi uliopita kama pesa pungufu hakuna picha utakayoiona na ikiwa pesa ni nyingi utaendelea kuona kifurushi kilichoisha,hivyo ili uone kifurushi ambacho umekusudia kutokana na pesa uliyolipa unapaswa kubadili kifurushi kwa kufata mtindo niliouelekeza hapa!
Chagua king'amuzi chako hapo chini ili kupata maelezo ya kina:-
  • Azam tv Bofya Hapa kujua kuhusu jinsi ya kuhama kifurushi!
  • Dstv Bofya Hapa kujua jinsi ya kuhama kifurushi!
  • Startimes  Bofya Hapa kujua jinsi ya kuhama kifurushi!
  • zuku Bofya Hapa kujua jinsi ya kuhama kifurushi!
Kwa maelezo haya nadhani hakuna usumbufu utakaoupata tena
na  kwa maelezo zaidi no.yetu ni ile ile!
+255 789 476 655

Share:

Jun 10, 2016

SI LAZIMA KUTAFUTA FUNDI

Nilikwishasema na leo narejea tena inapotokea king'amuzi chako hakionyeshi la kufanya kwanza Bofya Hapa ukiona bado huelewi hebu fanya jitihada za kulifikia Dish lako ama Antenna yako!! Sasa kama hii Dish fundi atacharge pesa ya signal wakati ilikuwa ni kukata hayo matawi ya mpapai ama kuukata kabisa!
Ushauri wangu watumiaji wa Ving'amuzi mjiongeze mtuhitaji inapolazimika tu sio kwa kazi kama hizi ambazo wenyewe mnaweza kuzifanya,huwa sijisikii vema kufanya kazi ambayo situmii taaluma yangu mfano wa hii hapa!

Share:

May 15, 2016

JINSI YA KUUNGA COAXIAL CABLE ( SIGNAL CABLE )

Leo nimeonelea tuelekezane jambo hili ambalo limeshakuwa ni tatizo miongoni mwa watumiaji wengi wa ving'amuzi,lengo langu likiwa ni lile lile sote kwa pamoja tuhamie Digital huku tukiwa na ufahamu wa kutosha juu ya ulimwengu huu!
Sio jambo geni kuunga Cable ya Signal,ile Cable inayotoa Signal kutoka kwenye Dish ama Antenna kuleta kwenye king;amuzi chako na kila mtu huwa na sababu yake ya kuunga!
> Sababu zinazopelekea kuungwa kwa Coaxial Cable:-
  • Cable kuwa fupi
  • Cable kuchunika
  • Cable kukatika
Hakuna madhara katika kuunga Cable kikamilifu isipokuwa madhara yanaweza kutokea ikiwa itaungwa ndivyo sivyo,pia inashauriwa kuunga Cable si zaidi ya mara mbili!

A > Uungwaji wa kienyeji usiotakiwa ingawaje unatumiwa na wengi

 No.1

No.2

No.3

Uungwaji huu sio mzuri kiujumla kwakuwa licha ya kuwa na muonekano mbaya pia kuna uhai mdogo wa signal,mbaya zaidi inategemea umeweka wapi muungo huu,ikiwa utaweka kama ilivyo hii picha hapo chini ni dhahili umetengenezea mazingira ya kuingia maji na kupigwa jua hivyo maji yatatengeneza kutu na jua litabandua hiyo gundi hapo hivyo maisha ya Signal huishia hapo.Ingawaje hii wakati mwengine hufanywa na Wateja wenyewe lakini pia kuna mafundi hufanya hivi kusudi huku wakijua kitaaluma hii haipo ni moja kati ya kazi chafu zisizotakiwa.




B > Uungwaji mwengine wa kienyeji usiotakiwa ingawaje unaonekana una nafuu

 No.1

 No.2

 No.3

No.4

Uungwaji huu angalau kimuonekano hauleti picha mbaya na wakati mwengine ni ngumu kuonekana kama umeungwa,uungwaji huu unatofautiana kidogo na wa A huu unahitaji umakini kidogo kwakuwa ukijichanganya kidogo na kusababisha ukagusanisha nyaya hakuna mawasiliano yatakayo pita katika muunganiko huo.Uungaji wa A na B ni kawaida kupunguza signal ikiwa hujaunga vizuri.
NB: muungo A na muungo B unahitaji umakini ili nyaya zisigusane.

SIGNAL QUALITY
Unachopaswa kufanya ni hiki hapa toka kwangu:-

  • Kwanza ni lazima ununue vihusika vifuatavyo

  1. Joint
  2. F connector pic 2
Ambapo thamani yake vyote ni kuanzia 2000 mpaka 3000 ingawaje unaweza ukauziwa hata 10000 inategemea tu unanunua wapi?
  • Chuna Coaxial cable ya vizuri kwa mtindo huu kama inavyoonekana hapo chini
Hakikisha Center conductor haigusani na Outer conductor

Outer conductor unaupindia juu ya jacket kama unavyoona hii picha

Outer conductor inakuja kugusana na Connector utakayoifunga isipokuwa Center conductor haitakiwi igusane na connector
  • Jinsi JOINT inavyofungwa na kufanya kazi






NB:Uungwaji wote wa Cable hakikisha Center conductor haigusani na Outer conductor.

mustaphamadish@gmail.com
+255 789 476 655
Share:

Apr 15, 2016

AV CABLE NI NINI!?


A inasimama badala ya Audio - Sauti
V inasimama badala ya Video - Picha
Zinakuwa nyaya tatu zenye rangi tatu tofauti:-


Nyekundu - Sauti Kulia
Nyeupe - Sauti Kushoto
Nyano - Picha


Hivyo tafsiri nyepesi ni kwamba AV CABLE ni waya unaosafirisha Sauti na Picha kutoka kwenye kifaa chochote kinachoweza kutoa picha na sauti na kuingiza kwenye TV, kifaa hicho kinaweza kuwa DVD, King'amuzi, game n.k.
Mfumo wa picha unaoonekana kwa kutumia AV cable hujulikana kama SD - Standard Definition 
 

Cable hii hutumika kwenye TV yenye AV Port yaani ile sehemu ya kuchomekea AV ambapo napo unachomeka kwa kufata rangi kama uvyoona hapo chini!


Zipo tv ambazo hazina AV port ama hicho kifaa ambacho unataka kutumia AV cable hakina AV Port ufanye nini ili uweze kuendelea kutumia AV cable ama Cable nyengine?
Unapaswa uangalie TV/DVD/King'amuzi kina Port gani badala ya AV Port?
Ufanye nini ikiwa TV yako ina AV port moja ama mbili nawe una vifaa zaidi ya viwili unataka kutumia pasipo kuchomoa chomoa AV cable?
Unapaswa kutumia kifaa kinachoitwa AV SELECTOR
mustaphamadish@gmail.com
+255789476655
Share:

Apr 12, 2016

KOPO HALISAIDII CHOCHOTE KWENYE DISH


Leo nimeonelea niongelee hili jambo kwakuwa ukiachilia kuliona sehemu mbali mbali pia nimekuwa nikulizwa kama kuna umuhimu wa wenye ving'amuzi vya madish kuweka makopo?
 Jambo la awali la kuzingatia king'amuzi kiwe cha Dish ama Antenna kina namna ya ufungaji wake kwa kutumia vifaa vyote vilivyomo kwenye set ya king'amuzi hicho,ikitokea kimojawapo umekiacha ndipo unajikuta nafasi ya kile ulichokiacha inachukuliwa na KOPO!
Kutumia KOPO kunatokana na sababu hizi:-
  • Tuanze kiufundi
- Fundi hupaswi kuacha kutumia kitu chochote kati ya ulivyovikuta kwenye set ya Dish kwakuwa vyote vina kazi yake na ni muhimu sana.

Hapa unamshawishi mteja atafute kopo lilipo ili aweze kufunika akiamini atasaidia angalau kuepusha gharama za kuita ita fundi.

Ukifunga hivi ni kipi ambacho kitamshawishi mteja aongezee ufundi wake wa kuweka kopo?
Fikra za watanzania wengi wanaamini wakifunika na kopo husaidia:-
  • Huzuia kunguru kufanya uharibifu
  • Husaidia picha kutokupotea wakati wa mvua
Niseme tu ukweli KOPO halisaidii chochoteikiwa fundi amefanyakazi safi.
Kupotea kwa Picha kwa dish ndogo kipindi cha mvua ni kawaida kutokana na uwezo mdogo ili kuepuka hili inakulazimu kutumia Dish kubwa ama lnb maalum na kuhusu kunguru fundi akifanyakazi yake vema kunguru hata abembee vipi hawezi kufanya uharibifu!
mustaphamadish@gmail.com
Share:

UMELIPIA NA BADO HUPATI PICHA!?


Hili ni janga kubwa karibia kwa wateja wote wa ving'amuzi vya kulipia,unafanya malipo lakini hupati picha kwa wakti ama hupati picha kabisa!
Njia za kufanya ili usipate usumbufu wakati wa kufanya malipo ya mwezi:-
> Kabla ya kufanya malipo hakikisha unajua bei ya kifurushi unachotaka kulipia
> King'amuzi chako umekiwasha kabla hujafanya malipo
> Ikiwa unalipia kifurushi ambacho ni tofauti na cha awali huna budi kupiga simu ama kufata njia zilizoelekezwa ili kubadili kifurushi
> King'amuzi chako kina Signal ya kutosha

Nini ufanye ikiwa umeshalipia na hukufata njia hizo:-
> Washa king'amuzi chako
> Hakikisha kina Signal kwa kuangalia channel ambayo ipo bure ( mf:ya matangazo )
> Piga simu kwenye kampuni husika ya king'amuzi unachotumia ili ufunguliwe ama upewe maelekezo zaidi na ikitokea umekosa msaada namba hii ni msaada kwako +255789476655
mustaphamadish@gmail.com
Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita