Kwanza ukishakuwa Fundi moja kwa moja unaaminika kwa taaluma
uliyonayo hivyo mteja ama jamii kwa ujumla wanajikuta wanaona unachofanya ama
kusema ndicho sahihi kutokana na wadhifa wako hata kama ni cha uongo… Binafsi
niwape angalizo wateja na mafundi kiujumla kwanza nianze na Wateja
Wateja – Nichukue nafasi hii kuwapongeza na kuwashukuru wale
wote wanaoheshimu na kuthamini uwepo wa Mafundi . Pia nichukue nafasi hii
kuwapa angalizo wale wateja wote wenye Dharau kwa kuona Mafundi si chochote ama
kudharau kile tufanyacho,Mfano mteja anahitaji fundi mnazungumza habari za
gharama na mnakubaliana,fundi anafika kwako na anafanyakazi yake kwa muda
mchache anamaliza kutengeneza..Mteja kwenye malipo unataka upunguziwe kwakuwa
kazi yenyewe ndogo tu ,hii ndo dharau nisiyoipenda hata kuisikia.. sasa kama
kazi ni ndogo tu kwanini hukufanya mwenyewe!? Hivi hujui kwanini imekuwa kazi
ndogo tu!? Kwakuwa ni Fundi ( Ufundi ni taaluma ) si kila mtu ana taaluma na ndo
maana ukahitaji Fundi.. Hivyo tumia lugha nyengine katika kutafuta unafuu wa
malipo lakini si kudharau kazi za watu. Mpe uhuru fundi afanye kazi yake si
kumbana hata anakosa kuwa comfortable maana fundi akiamua kukufanyia uhuni hata
ukienda nae mguu kwa mguu ana nafasi 99% ya kukufanyia uhuni.
Mafundi – Lazima ujielewe kama si kuelewa thamani yako,ujue
uwezo wako pia maana kuwa Fundi si kigezo cha kujua kila kitu ingawaje wapo
mafundi kwa taaluma yake anajua kila kinachomuhusu.. hii maana yake kama umekutana
na Technical issue ambayo kwako ni ngeni omba msaada kwa mafundi waliokuzidi
ama ukikosa msaada mwambie mteja wako ukweli kwamba hilo tatizo huwezi
kulisolve.. Kamwe usiseme uongo ili tu upate pesa.. Hakikisha unakuwa makini
katika kazi yako,akili yako uiweke kwenye kazi uifanyayo wakati wa kazi ili
isitokee ukafanya usahaulifu wowote maana utakuwa ni uzembe na matokeo yake
itakucost ila zaidi itamcost mteja wako… mfano hii picha hapa chini
Kosa dogo alilofanya limesababisha huu mkono wa dish la DStv
kuliwa na kutu kwakuwa hakuweka kifuniko ambacho kinazuia maji kuingia ndani ya
mkono huu wa kushika Lnb..
hili ni kosa dogo kimtazamo ila kiufundi ni kosa
kubwa sana linaweza likawa limefanywa na fundi kwa bahati mbaya ama kwa
makusudi kwa kudharau vile vifuniko vya kufunikia hii mikono.. Amedril vizuri
na amefunga cable vizuri lakini kilichomshusha vyeo kuonekana ni fundi kalipua
ni kosa moja tu…
Tuna Mafundi wataalamu wa kufunga
-
Azam TV
-
DStv
-
Zuku Tv
-
StarTimes
-
Continental
-
Ting
-
Flat Screen
-
Projector
-
CCTV Cameras
Waliobobea kufunga kwenye:
-
Hotel
-
Apartment
-
Bar
-
Restaurant
-
Office
-
Majumbani
Tunapatikana Dar es salaam, Magomeni Mapipa.. isipokuwa mkoa wowote Tanzania
tunakuja.. inategemea unataka huduma gani toka kwetu!
Piga +255678476655