Call / WhatsApp +255673378129

Nov 3, 2014

USISUMBUKE | PIGA +255658046655 | TUNAKUFATA ULIPO

Nilichogundua ni kwamba nina wadau wengi sana ambao haipiti siku bila kutembelea haka kablog chetu na kupata mawili matatu kuhusu ukanda huu..
Wengi mnataka kujua habari za ving'amuzi na huduma kwa ujumla..
Ufumbuzi wa ving'amuzi vyote upo kwenye haka kablog,maana yake ukishindwa kuelewa simu inahusika,ukipiga tu jua shida yako imeisha!


KWA KUWAJALI WATU WANGU...
Nimeanzisha huduma ambayo haikupi usumbufu na ni rahisi kwako!
Natekeleza maana ya huduma mtandaoni,kama tujuavyo huu ni wakati wa Digital hivyo lazima twende kidigital zaidi...
Swali unapenda/unataka king'amuzi gani kati ya hivi:-
DStv/Azam tv/Digitek/Continental/Zuku tv/Star times.
Piga simu sema unataka kipi,tunakupa ushauri na kisha utaletewa mpaka ulipo
Tukifika unalipia na kufungiwa papo hapo!
Ila hii ni kwa wakazi wa Dar es salaam tu!
Piga sasa +255784378129
TUMEBOBEA KUFUNGA KWENYE:-
HOTEL/APARTMENT/MAOFISINI NA MAJUMBANI.
BAADHI YA WALIONUFAIKA NA HUDUMA ZA MUSTAPHA MADISH:-
TRANSIT MOTEL/JB BELMONT/GERRAFE VIEW HOTEL/IKULU-OFFICE YA WAZIRI MKUU/PSPF/BAHARI BEACH LODGE/N.K.
Share:

Nov 1, 2014

HDMI CABLE


Imenipelekea kuandika post hii kutokana na simu niliyoipokea hivi karibuni kutoka Dodoma,lakini kabla ya simu hiyo kuwaelewesha wadau wangu kuhusu HDMI CABLE ni kawaida tu ila kwenye hii blog yetu leo wacha nitoe kile kidogo nilichonacho kwa wadau wangu!
Unapozungumzi HD
lazima ushirikishe cable inayoitwa HDMI CABLE,kwasababu ili uone picha katika mfumo wa HD ( Ubora wa picha wa hali ya juu ) ni lazima utumie HDMI CABLE,cable ambayo inatoa picha kutoka kwenye inaweza kuwa DVD/Receiver/King'amuzi ama chochote chenye uwezo wa kutoa HD na kupeleka kwenye tv ambayo nayo ikiwa ina uwezo wa kupokea HD.



Hii cable inachomekwa kwenye tundu lililoandikwa HDMI.
Ili kujua kama tv/DVD ama king'amuzi chako ni HD unapaswa kuangalia kwa umakini je kuna tundu lililoandikwa HDMI,kama lipo hilo jua kifaa chako hicho ni HD.
Je unavijua ving'amuzi vilivyo kwenye mfumo wa HD hapa Tanzania..??

  Una swali  piga +255789476655
Share:

Oct 29, 2014

DSTV PACKAGES | VIFURUSHI VYA DSTV


Lengo la kuwa na vifurushi tofauti ni kutoa fulsa kwa kila mdau kuweza kununua na kufanya malipo ya mwezi kutokana na uwezo wake.
Hivi ndivyo vifurushi vya DStv,idadi ya channel na bei kwa ujumla:-

1-DSTV BOMBA PACKAGE
Ina channel 65+ bora
Bei mpya ni Tsh 19,000
Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!

2-DSTV FAMILY PACKAGE
Ina channel 70+ bora
Bei mpya ni Tsh 39,000
Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!

3-DSTV COMPACT PACKAGE
Ina channel 85+ bora
Bei mpya ni Tsh 69,000
Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!

4-DSTV COMPACT PLUS PACKAGE
Ina channel 90+ bora
Bei mpya ni Tsh 109,000
Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!

5-DSTV PREMIUM PACKAGE
Ina channel 120+ bora
Bei mpya ni Tsh 169,000
Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!

CHANNEL MAALUM | BEI ZAKE

DStv French Touch
Ina channel 7 bora
Malipo ni Tsh 15,600
kujua channel zilizopo!


DStv Indian
Ina channel 4 bora
Malipo ni Tsh 71,500
kujua channel zilizopo!


DStv French Plus
Ina channel 15 bora
Malipo ni Tsh 88,000
kujua channel zilizopo!


DStv Great Wall China
Ina channel 10 bora
Malipo ni Tsh 16,500
kujua channel zilizopo



JINSI YA KUHAMA KIFURUSHI Bofya Hapa


  Mafundi wa DStv | Chochote kuhusu DStv | +255 789 476 655
Share:

Oct 27, 2014

VING'AMUZI VISIVYO NA MALIPO

Nilichogundua ni kwamba watanzania wengi wanapenda ving'amuzi rahisi,rahisi kwenye kununua na katika ulipaji wa kila mwezi na pindi linapotokea swala la kutokuwa na malipo ya mwezi inakuwa ndio unafuu zaidi,kwasababu wanzania wengi wenzangu na mie...
DIGITEK

Hiki hakina malipo ya mwezi kwa mujibu wa wao wenyewe,ukinunua kwa tsh 110,000/= 
Inakuwa umemaliza labda gharama yako itazidi ikiwa unahitaji na Antenna.
CONTINENTAL

Hiki nacho sio kama hakina ila kipo hivi,ukinunua unaangalia na kuanza kulipia baada ya miezi 12 yaani mwaka mmoja,ingawaje mpaka sasa malipo hayajaanza kufanyika.
Ya Antenna tsh 75000/=
Ya Dish tsh 105000/=

TULIPOTOKEA....
TING pia haikuwa na malipo ya mwezi ilikuwa ukinunua umenunua,lakini sasa malipo mwanzo mwisho...

MAONI | USHAURI | HUDUMA | +255789476655
Share:

Oct 26, 2014

UNATAKA AZAM TV? | TUNAKUFATA | UNALIPIA | UNAFUNGIWA PAPO HAPO!

Hapa tunazungumzia malipo ya mwezi ni Tsh 12500/=
Unapata jumla ya channel 60.
Ukitaka kuzijua bofya hapa
Huduma hii inaweza kukufata popote ulipo ndani ya dar es salaam na malipo ukafanyia nyumbani ama mahali ulipo kabla ya kufungiwa king'amuzi chako.
Hii itakurahisishia wewe kutokusumbuka!
Hii yote ni katika kuboresha huduma zetu na kukuweka karibu yetu.
Kazi hii ni moja kati ya waliolipia nyumbani!




Unataka tukufate ulipo,ama tatizo lolote kuhusu azam tv?
+255789476655 Mustapha.
Share:

Oct 16, 2014

NAWALETEA CONTINENTAL YA DISH


Hatimae marejeo yamekuwa mazuri,ambapo sasa macho ya watanzania na wadau wa ving'amuzi kwa ujumla yameelekezwa kwa Digitek kuona yakuwa nao watatoa dish baada ya Continental kutoa Dish!
Hii inamaanisha leo ukihitaji king'amuzi cha Continental nitakachokuuliza cha kwanza..
unataka Continental ya Antenna ama ya Dish..
kisha mengine yanafata..

Share:

UWEZO BINAFSI

Ijapokuwa imepita miezi ipatayo 10 ila hili ni moja kati ya niyakumbukayo na ya kujivunia pia na sababu napokea simu mpaka wakati mwengine naona imepitiliza ila kwakuwa ndo kazi yangu sinabudi kumaliza shida za wadau wangu...
Nakumbuka ni maeneo ya sinza pale kumekucha kwa mzee moja hivii wa kihindi nilifunga Azam tv,kama ilivyoada kulipua kwangu ni mwiko nikafanya yangu na kanuni zangu kisha nikakabidhi kazi kwa mteja wangu!
Mteja cha kwanza kuniambia "nimependa kazi yako,umechukua muda mfupi na kazi safi" kwa kulithibitisha hilo wakamtoka wekundu wekundu pale nje ya malipo ya king'amuzi,hii alitoa kama pongezi yake kwang,nami kwakuwa nimetumwa helaa aaah nikashukuru pale wekundu wangu mfukoni kisha nikachapa mwendo!
ilipita kama wiki mbili alipata tatizo la king'amuzi maana kulikuwa na fundi akaleta ufundi nyumbani kwake hivyo alitaka msaada wa fundi,ilimlazimu afike ofisini na kwa bahati mbaya sikuwepo..fundi aliyepo akachukua nafasi yake akaenda na mteja kuangalia tatizo...
Tatizo alilimaliza na mteja akaendelea pata burudani kama kawaida...
Ikapita kama siku kadhaa tu mbele akaja tena ofisini kwa kununua king'amuzi kingine ila kwasasa alitaka zuku lakini safari hii pia hakunikuta,alidai aondoke na vifaa vyake ila kufungiwa anataka afungiwe na Mustapha,nilijaribu kupigiwa simu nami nilisema ukweli ni kama baada ya siku nne ndipo nitakuwa na muda,kitu ambacho kila mmoja pale ofisini alishangaa kuona mteja anakubali kuningoja..
Haikuchukua siku nne bali yule mteja alingoja kama wiki na siku tatu ndipo nikapata muda wa kwenda kumfungia Zuku yake..
Na hapo ndipo nikapata malalamiko ya fundi aliyeenda kufanya repair baada ya kupita mimi..
Hakukuwa na maelewano mazuri,lugha ya biashara haikutumika hapa ila nilichofanya ni kumtaka radhi kisha nikampa burudani kama ilivyo ada!
Matokeo yake hataki fundi yeyote zaidi Mustapha.
Hapa tunazungumzia uwezo binafsi si kama najua saana,ijapokuwa najua vilivyo vingi ukanda wangu na hata aliyefanya hivyo ni mwanafunzi wangu kati ya wanafunzi wangu wengi tu ila alishindwa ama wanashindwa kufata ile misingi husika..
Mafanikio huja kwa kupenda unachofanya!
Ukipenda unachofanya,utakifanya kwa uwezo wako wote na hii lazima ufanikiwe..
Upo facebook Bofya hapa like page yangu kupata mapya ya ving'amuzi vyote Tanzania
Share:

Oct 13, 2014

HII SIO SAWA KABISA

...nilipoona Dish hii ya DStv wala sikushangaa sana na badala yake ndipo nikaamua kupiga picha ili alau kile ambacho nilichokuwa sijawahi hata kukumbusha tukumbushane kwa pande zote mbili..
Mafundi wenzangu na wateja wetu pia wote wa ving'amuzi kwa ujumla hasa vile vya kutumia Satellite Dish.
Nianze na mafundi wenzangu wataalam wa madish... 
Inawezekana ukawa na kazi nyingi na inakulazimu ukifika site -kwa mteja,huwa huitaji kutumia muda mwingi bila kuangalia kama kazi unayoifanya itakuwa nzuri ama laa,matokeo yake unalipua tu ili mteja aone tu kwa wakati huo nawe uchukue chako na kesho akuite tena...
Kitaaluma hii si sawa hata kidogo..
Yaani kama umemuibia mteja wako..
Madhara ya hii licha ya kuonekana fundi mbabaishaji pia hautaweza kupata wateja wengine kupitia wateja uliowafanyia uhuni huu!!

Hakuna tangazo zuri kama kupitia kwa mteja uliyemuhudumia vema,labda nikwambie kitu ijapokuwa hii blog inanipa wateja lakini si kama ufikiriavyo wateja wangu wengi wanatokana na wale niliowahudumia vizuri na hii ndio siri ya mafanikio yangu katika taaluma hii..

Ila nilichogundua wateja wengi hasa wanawake si wasichana si wamama wao shida yao kubwa ni kuona tv inaonyesha,ila swala umefunga wapi hilo utajua fundi.
Wateja wetu wapendwa..

Share:

Oct 12, 2014

KING'AMUZI CHA BEI RAHISI KULIKO VYOTE TANZANIA

Swali?
Je unahitaji urahisi wa kulipa malipo ya mwezi ama kununua..!?
Limekuwa kama tatizo hivi kwa nchi yetu toka lilipokuja swala la udigital kuingia na kulazimika kila aliye Tanzania ili uangalie tv ni lazima king'amuzi kihusike!
Issue inakuwa hapa kuhusu king'amuzi!!
Kipi ni bei rahisi na kizuri kinachomfaa mtanzania na hata asiye mtanzania kwa ujumla!
Kipi ni king'amuzi bei rahisi swali la jibu hilo unaweza ukawa nalo wewe ila mimi wajibu wangu ni kukuletea bei za ving'amuzi vyote kisha wewe ndio mchaguzi kutokana na kipato chako na upenzi wa channel kwa king'amuzi husika..
DSTV TSH 99,000/= BEI YA OFFER BILA UFUNDI.
BEI YA SASA DSTV Bofya hapa
Hii sio bei ya siku zote,bei hii ni maalum kwa offer tu na pindi offer itakapoisha bei kamili nitawaletea!
 Baada ya hapo unachagua kifurushi ili ulipie uweze kuona Bofya hapa
Angalizo:Malipo ya mwezi yanapanda ama kupungua kutokana na dollar.

ZUKU TV TSH 75000/= BILA UFUNDI
Ambapo ukinunua unapata na mwezi mmoja bure!
 Baada ya mwezi wa offer kuisha unachagua kifurushi ili uendelee kuona Bofya hapa

AZAM TV TSH 135000/=
BEI YA SASA AZAM TV 

Kwasasa bei ya Azam tv ni tsh 135000 bila kufungiwa wala kifurushi.
Kufungiwa ni tsh 30,000/=
Vifurushi ni:- Bofya hapa

STARTIMES TSH DISH
STARTIMES TSH  ANTENNA
Hivi karibuni kimeanza cha dish,lakini hii haina maana kuwa cha antenna hakifanyi kazi kipo kama kawaida.
Vifurushi vya startimes ni:- Bofya hapa

DIGITEK TSH
Hii haina malipo ya mwezi ukinunua inakuwa ndio umenunua!
Lakini kutoka hapa kwangu na mtazamo wangu nitakuja kuzungumza kuhusu ving'amuzi visivyokuwa na malipo ya mwezi.

CONTINENTAL TSH 145000/=
Hiki nacho hakina malipo ya mwezi ukinunua umenunua.
Kujua channel zilizopo Bofya hapa

EASY TV TSH
Hiki kwa mwezi ni tsh 10,000/=

TING TSH 125000 DISH
 Tsh 20000/= ch100

TING TSH 60000 ANTENNA 
Vifurushi tsh 8000/= ch18+
16000 ch40+

Post hii itaboreshwa......

+ 255 789 47 66 55
Share:

Oct 11, 2014

STARTIMES YA DISH

King'amuzi ambacho kilipoanza kilipokelewa vizuri sana,watanzania wengi walinunua ila baadae kidogo kulitokea tatizo,tatizo ambalo liliwaweka wakati mgumu sana hasa katika kupata wateja wapya na wale wa zamani kutafuta namna ya kuondokana na tatizo hilo..
Tatizo la signal ambalo lilipelekea picha kukata kata ama kupotea kabisa ila ambalo lililokuwa linatokea hata kama mteja hajafunga vizuri Antena yake ama mafundi ambao wateja wanawatafuta ili wafungiwe Antanna zao kufunga ndivyo sivyo lakini atakachomalizia kusema tatizo ni la star times wenyewe..
Tatizo ambalo walikabiliana nalo na kulimaliza kabisa na kama inatokea kwa sasa zungumza na fundi wako ila kama ni fundi wewe mwenyewe maana watanzania tunaongoza kwa kuingilia kazi za watu..unapaswa Antanna yako kuielekeza Makongo juu,tatizo likiendelea hebu angalia cable yako ipo sawa? hakuna sehemu iliyochubuka kama sio kukatika? 
Likizidi hapo kuna namna unaweza nicheck nikakusaidia!
Binafsi huwa nasema Digital ni Dish ila inapotumika Antenna naona bado Analogue!
Pongezi kwenu Star times Tanzania kwa kuboresha huduma zenu kwa kuleta startimes ya dish,hili ni jambo zuri sana kwenu na kwa wateja wenu kwa ujumla!
Kwa tsh 105000/= umepata star times ya dish
Ambayo inakuwa na kifurushi cha mwezi mmoja ndani
Kwa maelezo zaidi na kuunganishwa +255789476655
Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita