Call / WhatsApp +255673378129

May 11, 2015

VING'AMUZI VINAVYOCHUANA | AZAM TV & DSTV | KIPI NI ZAIDI!?


Dstv ni wakongwe hii haina ubishi,ila ukongwe wa dstv haina maana kuwa hakuna king'amuzi ambacho kinaweza kuja na kufanya vizuri zaidi yake,hii inatokana na kwanza kujua mahitaji ya watazamaji kwa ujumla na kuwatimizia kile wanachokihitaji,unafuu wa bei ukizingatiwa.
Azam tv ni king'amuzi kipya kati ya vyote unavyoviona ila ndio king'amuzi kinachokimbizana na wakongwe,kwanini? kwasababu wameangalia watazamaji wanataka nini na kwa unafuu pia..Ingawaje Azam tv haijakidhi mahitaji wa wadau kwa 100% lakini alau wameweza kwa ukubwa.
Wadau wengi ni wapenzi wa mpira hivyo Azam tv wamefanikiwa kwa mpira wa Tanzania na Dstv bado anang'ang'ania ukongwe wake kwa mpira wa nje.
Ving'amuzi hivi vina mapungufu yake na kinachowakera wengi ni haya hapa:-

MAPUNGUFU YA DSTV
-Kubwa linalolalamikiwa na watanzania wengi ni bei kuwa juu,nikimaanisha malipo ya mwezi na hii inachangia na mtindo unaotumika wa kutumia $ badala ya Tsh.
Madhara ya kuwa bei juu kumefanya wadau watafute kila aina ya njia kuona wanapata uhondo wa dstv ila kwa njia isiyo rasmi,na hii inapelekea kupunguza walipaji halali wa malipo ya mwezi.
-Wana local channel,lakini malipo ya mwezi yanapokata hawaziachi zikawa bure.
Hayo ni mapungufu makubwa kwa Dstv.

MAPUNGUFU YA AZAM TV
-System wanayotumia kushindwa kutambua malipo ya mwezi wanayolipia wateja na kufunguka badala yake ukilipia kifurushi ukipendacho mpaka upige simu,hii imekuwa kero kwa wateja wengi wa azam tv,mteja anakaa mpaka wiki mbili na ikitokea hapigi simu unapita mwezi pasi kuona kile kifurushi alicholipia.
-Mawakala na wauzaji wengine wasio mawakala kuuza bei tofauti na bei sahihi.Hii sio tu mikoani ijapokuwa mikoani lawama hizi ni kubwa lakini hata hapa Dar es salaam wapo wanaouza bei juu tofauti na matangazo yalivyo.
-Picha kupotea kipindi cha mvua,king'amuzi ambacho kinaongoza kwa kupotea signal wakati wa mvua ndogo tu,hii ni kero nyengine kubwa kwa wateja wa Azam tv,kitaalamu hii inatokana na signal kuwa chini hivyo ni jukumu la Azam tv kuongeza signal badala ya 60 zifike alau 80 lakini kinachotakiwa mfikishe 100.
Hayo ni mapungufu makubwa kwa Azam tv.
TOFAUTI KUBWA KATI YA DSTV & AZAM TV
Dstv ana huduma zaidi ya moja kama:-
Extra view-Inakuwezesha kuona channel mbili tofauti kwa tv mbili tofauti kwa a/c moja.
Explora-Inakupa fulsa ya kurecodi saa 150 na mengineyo.
Umiliki na utofauti wa channel.
Dstv inaonyesha mpira wa nje na Azam tv mpira wa ndani.

MUSTAPHA MADISH | +255789476655 | mustaphamadish@gmail.com
Share:

May 1, 2015

STAR TV | AZAM TV | PAMOJA SASA

Awali ilikuwa ili kupata Star tv kwenye king'amuzi cha Azam ilikuwa ni fundi na ufundi wetu tu,kwani ilikuwa tunafunga satellite mbili kwa wakati mmoja ila baadae wenye mali yao hapo Satellite ya Amos 5 wakafanya ya kufanya.
Baada ya vuta nikuvute hatimae sasa Star tv imeungana na Azam tv,hivyo jambo hili limepelekea kila mmiliki wa king'amuzi cha Azam alipokee kwa furaha,huku wale ambao walikuwa wanasita kujiunga na Azam kwasababu hakuna Star tv huu ndo wakati wenu labda mseme lengine.

+255789476655 | HUDUMA ZA AZAM TV
Share:

Apr 27, 2015

MVUA NA VING'AMUZI VYETU


Kwa kawaida mvua inapokuwa inanyesha watu wengi nami nikiwa mmojawapo huwa mapenzi yapo kukaa sehemu tulivu kama panaruhusu unaangalia tv,iwe ni movie ama vyovyote vile ijapokuwa mimi mapenzi yangu kuangalia movie...
Ikiwa una king'amuzi chako na unataka kuangalia huku ukipisha mvua ifanye yake kisha uendelee na ratiba zako..King'amuzi nacho kinagoma kutoa picha..Mvua inaponyesha ving'amuzi vinavyotumia dish ndogo huwa vinaelemewa ila inapokata mvua navyo vinaonyesha picha kama kawaida..Unadhani ni kwanini vinaelemewa? Fuatana nami..






Share:

Apr 14, 2015

VING'AMUZI VYA ANTENNA


EASY TV
King'amuzi cha kwanza cha antenna ambacho mpaka sasa kipo ila kiukweli kama wanasua sua na kujikuta kila kukicha wanapoteza wateja badala ya kuongeza wateja.
Sababu ya king'amuzi hiki kupoteza wateja kila kukicha ni kutokana kukosa kuwapa uhakika wateja wao na wale wateja wapya,ambapo hata huduma zitolewazo kama zina usiri matokeo yake kimekuwa king'amuzi ambacho hakijulikani na watanzania wengi,pia kingine kinachowakimbiza wateja ni namna channel zinavyopungua kila kukicha ijapokuwa kuna ambazo zinaongezeka!
Pamoja na hayo yote malipo ya mwezi ni  tsh 10,000/= toka walipoanza mpaka sasa.


STARTIMES
Katika zile mbio za kuingia katika mfumo wa digital,ndipo kikazaliwa king'amuzi hiki ambapo kuna ushirikiano kati ya tanzania na china,hivyo kwa lugha nyepesi hiki ndicho king'amuzi cha TBC na hiki ndicho king'amuzi pekee unachoweza kupata TBC2.
Ingawaje king'amuzi hiki kilianza katika mfumo wa transmeter kwa lugha nyepesi kutumia antenna lakini sasa wameingia kwenye mfumo wa satellite pia mfumo wa dish hivyo kuwa ni kati ya vile ving'amuzi vichache vinavyotumia antenna na dish pia ila kwa decoder tofauti.

TING
Hiki king'amuzi ni mali ya taasisi ya dini,sababu hiyo imepelekea kuwa na idadi ya channel nyingi za dini zikiwemo za ndani na nje ya nchi.
Ingawaje nacho kilianza na antenna lakini baadae kikaongeza kutumia mfumo wa dish,hivyo kuna decoder aina mbili za antenna na za dish pia.

DIGITEK
Kulikuwa na  ile kila kampuni inayomiliki vituo vya tv kutaka kumiliki ving'amuzi vyao,na hii ilipelekea watanzania kuongea saana kwamba tutanunua ving'amuzi vingapi ila kuna baadhi ya makampuni wakaachana na habari hiyo ila makampuni mengine yakatimiza azma yao na katika kuthibitisha hili kikazaliwa king'amuzi hiki,
Ambacho walifanya hawakuwa na malipo ya mwezi,ilikuwa ukinunua wewe ni kutumia tu ambapo mpaka sasa.
King'amuzi hiki kikapotea,vilikuwa vimeisha huku fununu zikiwa wanaleta ving'amuzi vya kutumia satellite kama vilivyo ving'amuzi vyengine,kweli hatimae wakatoa decoder zenye uwezo wa kusoma antenna na dish.

CONTINENTAL
Katika kule kila kampuni kumiliki king'amuzi chake,star tv wameingia kwenye orodha hiyo kwa kumiliki king'amuzi hiki.Ambapo kumezaa star tv zaidi ya moja kama star bunge,star music na nyenginezo ilihali kuleta tofauti na ving'amuzi vyengine na kuongeza umuhimu kwa watazamaji.
Antenna ilihusika sana huku wakiwa hawana malipo ya mwezi kama digitek,ilifikia hatua wakahitaji kubadili ule mfumo waliokuwa wanautumia katika kurusha matangazo yao hivyo iliwalazimu kupotea hewani huku wateja wao wasijue siku watakayorejea.
Sasa wapo hewani,wapo hewani huku wakiwa wameingia katika ule mfumo uliotazamiwa na wengi ambapo hivi sasa wanatumia Antenna na Dish pia.

VING'AMUZI VYOTE HIVI VINAINGILIANA ANTENNA
Nimejaribu kutumia picha ya antenna moja kwa ving'amuzi vyote kwa kuwa unaweza ukatumia antenna hiyo kwa ving'amuzi vyote bila shida!
Kuna baadhi ya maeneo unaweza ukatumia antenna ya ndani na ukapata picha vizuri tu ila kuna maeneo ni lazima uweke antenna ya nje na bomba lako liwe refu pia.



KUNUNUA KING'AMUZI | MAFUNDI | USHAURI | +255789476655

Share:

Apr 9, 2015

BEI MPYA ZA MALIPO YA MWEZI DSTV

Ikiwa wadau wapo katika kulala na kuomba angalau gharama za malipo ya mwezi zipungua,hali imekuwa tofauti kutokana na gharama za uendeshaji ambapo imepelekea kupanda kwa bei za malipo ya mwezi kwa vifushi vyote vya Dstv kama ifuatavyo:-

BOMBA PACKAGE 
Awali ilkuwa tsh 18,500
Ikabadilika na kuwa tsh 23,500
Ikabadilika tena na kuwa tsh 19,975
Ambapo sasa hii 2017 ni  Tsh 19,000
ukitaka kujua idadi na channel zilizopo Bofya Hapa

FAMILY PACKAGE
Awali ilkuwa tsh 40,000
Ikabadilika na kuwa  ths 51,000
Ikabadilika tena na kuwa tsh 42,900
Ambapo sasa hii 2017 ni  Tsh 39,000
ukitaka kujua idadi na channel zilizopo Bofya Hapa

COMPACT PACKAGE
 Awali ilkuwa tsh 66,000
Ikabadilika na kuwa  ths 84,500
Ikabadilika tena na kuwa tsh 82,250
Ambapo sasa hii 2017 ni  Tsh 69,000
kitaka kujua idadi na channel zilizopo Bofya Hapa

COMPACT PLUS PACKAGE
Awali ilkuwa tsh 113,000
Ikabadilika na kuwa  ths 147,000
Ikabadilika tena na kuwa tsh 122,500
Ambapo sasa hii 2017 ni  Tsh 109,000
ukitaka kujua idadi na channel zilizopo Bofya Hapa

PREMIUM PACKAGE
Awali ilkuwa tsh 199,000
Ikabadilika na kuwa  ths 219,000
Ikabadilika tena na kuwa tsh 184,000
Ambapo sasa hii 2017 ni  Tsh 169,000
ukitaka kujua idadi na channel zilizopo Bofya Hapa


HUDUMA ZA DSTV | MSAADA KIUFUNDI | +255789476655

Share:

Mar 27, 2015

VIFURUSHI VYA AZAM TV | AZAM TV PACKAGES


Awali hakukuwa na mfumo huu wa vifurushi ila kutokana na uendeshaji na kutafuta maboresho imepelekea kuanza mfumo huu wa vifurushi,katika kumbukumbu za wengi ndicho king'amuzi kilichokuwa quality,channels nyingi ila malipo ya mwezi ni madogo!
Hivi ndivyo vifurushi vya azam tv,idadi ya channel na bei:-

1.AZAM LITE PACKAGE
Ina channel 40+ bora
Malipo ni Tsh 10,000/= kwa mwezi
Malipo ni Tsh 3,000/= kwa wiki
Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!

2.AZAM PURE PACKAGE
Ina channel 60+ bora
Malipo ni Tsh 18,000/=
Malipo ni Tsh 7,000/= kwa wiki
Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!

3.AZAM PLUS PACKAGE
Ina channel 90+
Malipo ni Tsh 23,000/=
Bofya Hapa kujua channel zilizopo katika kifurushi hiki!

4.AZAM PLAY PACKAGE
Ina channel 105+
Malipo ni Tsh 28,000/=

MSAADA - KIUFUNDI | KUNUNUA | CHOCHOTE KUHUSU AZAM TV | 
+255 789 476 655
Share:

Mar 20, 2015

BEI ZA VING'AMUZI NJE YA DAR ES SALAAM

Kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu kuhusu bei za ving'amuzi katika mikoa yote ukiacha dar es salaam ijapokuwa baadhi ya wauzaji wa dar es salaam hili linawahusu!
Hapa nazungumzia ving'amuzi vyote vilivyopo tanzania,kampuni husika wanatoa bei elekezi ambapo bei hiyo inapaswa kuuzwa kwa mikoa yote tanzania bila kuongeza hata senti 5.
Unaweza ukaona ni jambo ambalo haliwezekani ila mimi najua ya kuwa inawezekana kama muuzaji ni wakala aliyeidhinishwa na kampuni hhusika.
Mfano wakala anaponunua azam tv kwa jumla anapata punguzo maalum na kuna utaratibu wa kurudishiwa pesa ya usafiri kwa kuzingatia mkoa gani anatoka,pia ving'amuzi vyengine wanautaratibu wao unaofafana na huo ili tu kufanikisha mawakala wote katika mikoa yote waweze kuuza bei elekezi na si vinginevyo!
Kinachotokea kutokujulikana kwa mawakala walioidhinishwa kwa baadhi ya mikoa kumesababisha wafanyabiashara kujiamulia kununua tu ving'amuzi na kuweka kwenye maduka yao na kujiuzia bei wanazotaka wao huku wakiwa hawajui vema kuhusu hivyo ving'amuzi,hii imepelekea malalamiko kuwa mengi kwa mteja kuchelewa kufunguliwa ili aweze kuona ama chochote kikitokea cha kiufundi aliyemuuzia anashindwa kumpa msaada unaostahiki kwa wakati.
Kwa maoni ushauri:+255789476655
Share:

Mar 1, 2015

BEI MPYA YA AZAM TV TSH 135,000/=


Hii ni kwa wateja wapya ambao wanataka kujiunga na azam tv,bei ya vifaa ni tsh 135,000/= hii namaanisha bila ufundi wala kifurushi!
Ili kufurahia huduma za azam tv inakupasa kufata utaratibu huu:-
VIFAA tsh 135,000/=
Inajumuisha Dish ikiwa na LNB,,Decoder ikiwa na smart card,cable mt20.
VIFURUSHI-
Azam pure tsh 12,000/= ch 25+
Azam plus tsh 20,000/= ch 50+
Azam play tsh 25,000/= zaidi ya ch 80
UFUNDI-
Ili ufungiwe inakupasa kulipa tsh 30,000/=
Hapa ndipo pana mvutano kidogo hapa,wateja wengi wanaona tsh 30,000/= ni nyingi na matokeo yake wengiwao wanaikwepa hii kwa kutafuta mafundi wao na kuwalipa chini ya 30,000 ama wanajikuta wanataka kufunga wenyewe matokeo yake wanaishia njiani kisha wanarudi tena kwetu!
Vipo vitu vya kujaribu lakini kitu kama ukijui tuachie tunaokijua,hii ina maanisha mgawanyiko wa kazi,madhara ya kuleta ufundi kufunga dish ikiwa hujui unaweza ukaua LNB ama ukaua Decoder.
1.Faida za kulipa tsh 30,000/= tukufungie sisi-
2.Ikiharibika ndani ya miezi mitatu repair bure.
Chochote kikitokea tunakusaidia kwa 100% kwa wakati.

Ukitaka kujua channels zilizopo kwenye kila kifurushi Bofya Hapa 

HUDUMA ZA AZAM TV | MSAADA KIUFUNDI | +255789476655
Share:

BEI MPYA YA DSTV TSH 99,000/= BILA UFUNDI


Baada ya ile offer ya tsh 99,000/=
Hii inajumuisha vifaa bila ufundi!
Kisha unachagua kifurushi ukipendacho kati ya hivi:-

KWA MAELEZO ZAIDI +255789476655

TUMEBOBEA KUFUNGA KWENYE:
HOTEL | APARTMENT | OFFICE
Share:

Feb 3, 2015

KIFURUSHI CHA AZAM PURE | AZAM PURE PACKAGE | TSH 18,000


Zijue channel zilizopo kwenye kifurushi cha azam pure:-
Kuna zaidi ya channel 60
  • Kwa wiki Tsh 7,000/=
  • Kwa mwezi Tsh 18,000/= 


Universal TV
BBS TV
Clouds TV Rwanda
Salam TV
Magic One
Channel 44
ASTV (Africa Swahili TV)
Boing
Africa News
Spark TV
TV - E
Salt TV
Baby First TV
Zodiak TV
Times TV
KASS TV
Jeem TV
MBC Plus Power
RAI Italia
Malawi National TV
KBC
Capital TV
Star TV
Azam Two
Azam One
KTN
K24
Bukedde TV 2
Rwanda TV
TV West
WBS
NBS TV
Urban TV
UBC
Citizen TV
EATV
ZBC 2
African Movie Channel
MBC 3
Liverpool TV
Manchester United TV
Real Madrid TV
Al Jazeera English
Fix & Foxi
Colors
MBC Bollywood
MTV India
ITV
Clouds TV
ZBC
Chanel 10
TBC1
Sinema Zetu
JINSI YA KUHAMA KIFURUSHI Bofya Hapa


KWA HUDUMA | USHAURI | CHOCHOTE KUHUSU AZAM TV | +255 789 476 655
Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita