EASY TV
King'amuzi cha kwanza cha antenna ambacho mpaka sasa kipo ila kiukweli kama wanasua sua na kujikuta kila kukicha wanapoteza wateja badala ya kuongeza wateja.
Sababu ya king'amuzi hiki kupoteza wateja kila kukicha ni kutokana kukosa kuwapa uhakika wateja wao na wale wateja wapya,ambapo hata huduma zitolewazo kama zina usiri matokeo yake kimekuwa king'amuzi ambacho hakijulikani na watanzania wengi,pia kingine kinachowakimbiza wateja ni namna channel zinavyopungua kila kukicha ijapokuwa kuna ambazo zinaongezeka!
Pamoja na hayo yote malipo ya mwezi ni tsh 10,000/= toka walipoanza mpaka sasa.
STARTIMES
Katika zile mbio za kuingia katika mfumo wa digital,ndipo kikazaliwa king'amuzi hiki ambapo kuna ushirikiano kati ya tanzania na china,hivyo kwa lugha nyepesi hiki ndicho king'amuzi cha TBC na hiki ndicho king'amuzi pekee unachoweza kupata TBC2.
Ingawaje king'amuzi hiki kilianza katika mfumo wa transmeter kwa lugha nyepesi kutumia antenna lakini sasa wameingia kwenye mfumo wa satellite pia mfumo wa dish hivyo kuwa ni kati ya vile ving'amuzi vichache vinavyotumia antenna na dish pia ila kwa decoder tofauti.
TING
Hiki king'amuzi ni mali ya taasisi ya dini,sababu hiyo imepelekea kuwa na idadi ya channel nyingi za dini zikiwemo za ndani na nje ya nchi.
Ingawaje nacho kilianza na antenna lakini baadae kikaongeza kutumia mfumo wa dish,hivyo kuna decoder aina mbili za antenna na za dish pia.
DIGITEK
Kulikuwa na ile kila kampuni inayomiliki vituo vya tv kutaka kumiliki ving'amuzi vyao,na hii ilipelekea watanzania kuongea saana kwamba tutanunua ving'amuzi vingapi ila kuna baadhi ya makampuni wakaachana na habari hiyo ila makampuni mengine yakatimiza azma yao na katika kuthibitisha hili kikazaliwa king'amuzi hiki,
Ambacho walifanya hawakuwa na malipo ya mwezi,ilikuwa ukinunua wewe ni kutumia tu ambapo mpaka sasa.
King'amuzi hiki kikapotea,vilikuwa vimeisha huku fununu zikiwa wanaleta ving'amuzi vya kutumia satellite kama vilivyo ving'amuzi vyengine,kweli hatimae wakatoa decoder zenye uwezo wa kusoma antenna na dish.
CONTINENTAL
Katika kule kila kampuni kumiliki king'amuzi chake,star tv wameingia kwenye orodha hiyo kwa kumiliki king'amuzi hiki.Ambapo kumezaa star tv zaidi ya moja kama star bunge,star music na nyenginezo ilihali kuleta tofauti na ving'amuzi vyengine na kuongeza umuhimu kwa watazamaji.
Antenna ilihusika sana huku wakiwa hawana malipo ya mwezi kama digitek,ilifikia hatua wakahitaji kubadili ule mfumo waliokuwa wanautumia katika kurusha matangazo yao hivyo iliwalazimu kupotea hewani huku wateja wao wasijue siku watakayorejea.
Sasa wapo hewani,wapo hewani huku wakiwa wameingia katika ule mfumo uliotazamiwa na wengi ambapo hivi sasa wanatumia Antenna na Dish pia.
VING'AMUZI VYOTE HIVI VINAINGILIANA ANTENNA
Nimejaribu kutumia picha ya antenna moja kwa ving'amuzi vyote kwa kuwa unaweza ukatumia antenna hiyo kwa ving'amuzi vyote bila shida!
Kuna baadhi ya maeneo unaweza ukatumia antenna ya ndani na ukapata picha vizuri tu ila kuna maeneo ni lazima uweke antenna ya nje na bomba lako liwe refu pia.
KUNUNUA KING'AMUZI | MAFUNDI | USHAURI | +255789476655