Baadhi ya ile team #FundiMakini mikono salama ya Mustapha MaDish na TeamKazi ikiwa inafanya Installation ya Flat Screen sehemu tofauti tofauti!
Si kila mtu anaweza kufanya tunachofanya!
Je unahitaji hii team ukuhudumie zaidi ya hivi?
Piga +255789476655
Kitu kizuri kwenye ulimwengu wa Digital Tv hususani kwa Tanzania kinakuja.. Lengo ni kusaidia watanzania wote kwa ukaribu zaidi kuhusu ulimwengu wa Ving'amuzi.. Kuna udhaifu mkubwa katika kutoa habari,msaada,ushauri nk. kwa jamii kuhusu ulimwengu wa Digital Tv.. Hii imepelekea kuwe na taarifa zisizo rasmi na kuendelea kuongopeana kila kukicha ama taarifa zinatoka kibiashara,unashawishiwa ili ununue king'amuzi fulani.. Mustapha MaDish na Team yangu lengo letu kuu ni kuhakikisha unaujua na unaufurahia ulimwengu wa Digital Tv...
Kuelekea kumaliza mwaka Zuku inakuja na Offer hii kwenye msimu huu wa sikukuu ya x mass na mwaka mpya !!
Tsh 88,000/= Kununua Badala ya Tsh 95,000/=
Hii unapata Vifaa vyote ( Dish,Decoder,Lnb na Cable )
Ndani yake unapata kifurshi cha Smart Pack kwa miezi mitatu buree!!
Hii ni bila ya Ufundi!
Ufundi ni Tsh 30,000/=
Jumla inakuwa ni Tsh 118,000/=
Ukiachilia OFFER hii kwa wateja wapya pia kuna punguzo la bei kwa Vifurushi karibu vyote ili kuendana na mfuko wako na ili kujua Vifurushi vilivyopo na bei mpya! Bofya Hapa
Mafundi wa uhakika wa king'amuzi chako unachotumia limekuwa tatizo kubwa hasa kwa baadhi ya maeneo,hii imepelekea baadhi ya wateja kuona yakwamba king'amuzi anachotumia ni tatizo kwakuwa hakupata Fundi makini ambaye angeweza kumfungia ama kumrekebishia ipasavyo.. Matokeo yake picha kuganda ganda ama kupotea ni jambo la kawaida sana..
Fundi Makini anapaswa kuwa na vifaa vilivyo kamilika ukiachilia spana zote muhimu pia anapaswa kuwa na Drill machine kwa ajili ya kutombolea na kingine anapaswa kuwa na kifaa cha kutafutia Signal ambacho kinaitwa Signal Finder!!
Fundi Makini akikufungia ama kukurekebishia atakupa uhakika wa miezi mitatu,maana yake ndani ya miezi mitatu baada ya kukitibu king'amuzi chako kikisumbua atakuja na kukurekebishia bure pasipo malizo yeyote!
Fundi Makini ni mwepesi kuja pale unapomuhitaji,tofauti na akina Fundi Kalipua ambao huwa ni ngumu sana kurudi ambapo ameshafanya kazi chafu!
Azam tv iliyofungwa na fundi kalipua ndo hiyo ya kwanza hapo na Azam tv inafungwa na Fundi makini ndo hiyo hapo inamaliziwa na mikono salama ya Chidy kuelekea Signal Quality Tv!
Kupata Moja ya Mafundi Makini wa Azam Tv Piga +255789476655
Achana na akina Fundi kalipua sehemu ya kudril wao wanapiga misumari,matokeo yake Signal inakuwa haina uhai ukija upepo picha inakatakata!
Ukifungiwa na sisi utapata miezi mitatu bure baada ya kufungiwa kama itasumbua utarekebishiwa pasipo kutoa gharama yeyote!
Wateja wengi wa Zuku tv wanakumbwa na kadhia hii,kutokujua utaratibu kwa
kutaka kuhama kutoka kifurushi kimoja kwenda kingine hivyo kwa post hii
utaelewa vema jinsi ya kuhama kifurushi!
Kwanza vijue Vifurushi vya Zuku tv kwa Kubofya Hapa
Ikitokea umelipia kifurushi cha Zuku Smart Pack Tsh 8,999 na mwezi umeshaisha
unataka kulipia kifurushi cha Zuku Classic Tsh 18,000 unaweza kufanya
hivyo kwa kufata utaratibi huu:-
Lipia kwanza Tsh 18,000 kisha chukua simu yako piga namba +255768984200 atakayepokea mwambie umelipia Tsh 18,000 kwa lengo la kutaka kuhama kifurushi hivyo akuhamishe.
Zoezi hili uhakikishe king'amuzi chako umekiwasha kisha ndipo unafanya
zoezi hili na inachukua dk 5 mpaka 30 kubadilik!
Tunaelekea kumaliza mwaka 2016 na kutokana na ushindani uliopo katika ukanda wa Digital tv,makampuni ya Ving'amuzi yanajitahidi kutafuta namna ya kushawishi wateja wapya na kujiunga na ving'amuzi vyao huku wakiwafanya wateja walionao kutowapoteza kwa kuboresha huduma zao na kutoa OFFER!!
Vijue Ving'amuzi vilivyo na OFFER na Offer zao kwasasa:-
Hii itakuwa ni habari nzuri kwa wateja wa DStv wapya na wale wa zamani Kwa kampuni ya Multichoice Tanzania kulifanya hili lililokuwa linawaumiza wengi kama sio kuwakimbiza!
Kuanzia terhe 1/11/2016 bei ya Vifurushi vya DStv itashuka na kuwa kama ifatavyo:-
DStv Premium Package Ni Tsh 219,000
Bei mpya itakuwa ni Tsh 184,000
Bofya Hapa Kujua channel zilizopo na bei mpya 2017
DStv Compact Plus Package Ni Tsh 147,000
Bei mpya itakuwa ni Tsh 122,500
Bofya Hapa Kujua channel zilizopo na bei mpya 2017
DStv Compact Package Ni Tsh 84,500
Bei mpya itakuwa ni Tsh 82,250
Bofya Hapa Kujua channel zilizopo na bei mpya 2017
DStv Family Package Ni Tsh 51,000
Bei mpya itakuwa ni Tsh 42,900
Bofya Hapa Kujua channel zilizopo na bei mpya 2017
DStv Bomba Package Ni Tsh 23,500
Bei mpya itakuwa ni Tsh 19,950
Bofya Hapa Kujua channel zilizopo na bei mpya 2017
Kupata msaada kiufundi na Mafundi wa DStv Bofya Hapa
Lipia kifurushi cha Azam Play Tsh 28,000/= kwa miezi 12 ( Mwaka mmoja ) ambapo ni Tsh , utapata Vifaa na Kufungiwa bureee!!!
Hii itakufanya uokoe Tsh 165,000/=
Offer hii iawahusu wateja wapya tu!
Kujua vifurushi na channels zilizopo kwenye Azam Tv Bofya Hapa
Kupata mafundi wa Azam TV Bofya Hapa
Kununua King'amuzi cha Azam Tv Bofya Hapa
Ile kununua kwa Tsh 79,000/= bado inaendelea ingawaje kwa sasa hakuna ile kupata na kifurushi cha Compact badala yake kuanzia Tarehe 1/11/2016 Vifurushi vyote vya DStv vitapungua bei..
Wateja wengi wa Startimes wanakumbwa na kadhia hii,kutokujua utaratibu kwa kutaka kuhama kutoka kifurushi kimoja kwenda kingine hivyo kwa post hii utaelewa vema jinsi ya kuhama kifurushi na utaondokana na ile adhabu ya kufanya malipio kwa lengo la kupata mwezi mzima matokeo yake unapata kuona kwa muda wa wiki 1 tu! Kwanza vijue Vifurushi vya Startimes kwa kubofya Hapa
Ikitokea umelipia kifurushi cha Smart Tsh 18,000 na mwezi umeshaisha unataka kulipia kifurushi cha Smart+SportPlus Tsh 32,000 unaweza kufanya hivyo kwa kufata utaratibi huu:-
Kabla ya kufanya malipo chukua simu yako bonyeza *150*63# kisha piga utapata ujumbe huu
Karibu StarTimes Chagua:
Kiswahili <
English
( Tunachagua kiswahili,una bofya OK )
Kujua salio
Kulipia kwa vocha
Sajili dekoda yako mpya
Q and A ( Swali na Jibu )
Chagua kifurushi <
( Unachagua "chagua kifurush,una bofya OK" )
Ujumbe utakaoupata ni:-
1.DTT ( Antenna )
2.DTH ( Dish ) <
Chagua kulingana na king'amuzi unachotumia,hapa nitachagua cha Dish
Ujumbe utakaoupata ni:-
Tafadhali ingiza tarakimu 11 za smati kadi yako iliyochomekwa upande wa kulia wa dekoda yako (mfano 02139xxxxxx )
( Weka namba za Smartcard yako zenye tarakimu 11,kisha una bofya OK )
Ujumbe utakaoupata ni:-
Smart-18k
Smart+SportPlus-32k <
Super-48k
( Unachagua unachotaka kulipia mfano tumechagua namba 2,una bofya OK )
Ujumbe utakaoupata ni:- Asante.Utapokea majibu hivi punde.StarTimes
NB:Niwe tu mkweli nilichelewa kuiweka hii post kwakuwa maelekezo yake kampuni husika imeshindwa kuyakamilisha hivyo najua ambacho mtapata ni usumbufu kwa maana hiyo utakapokwama huna budi kupiga +255764700800 ili uhamishwe kifurushi.
Kifurushi cha Smart Plus kimeongezeka huku beo zikiwa pungufu kwa baadhi ya vifurushi pia,mabadiliko hayo ni kama ifatavyo:-
1-ZUKU SMART PACK
Ina channel 30 tv safi.
Channel 18 radio.
+ Channel za Tanzana.
Malipo Tsh 8,999 kwa mwezi. Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!
2-SMART PLUS
Ina channel 40 tv safi.
Channel 18 radio.
+ Channel za Tanzana.
Malipo Tsh 13,000 kwa mwezi. Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki! 3-ZUKU CLASSIC
Ina channel 69 tv safi.
Channel 55 radio.
+ Channel za Tanzana.
Malipo Tsh 18,000 kwa mwezi.
Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!
4-ZUKU PREMIUM
Ina channel 98 tv safi.
Channel 55 radio.
+ Channel za Tanzana.
Malipo Tsh 25,000 kwa mwezi. Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!
5-ZUKU ASIA PACKAGE
Ina channel 26 safi.
Malipo ni Tsh 24,000 kwa mwezi. Bofya Hapa kujua channel zilizopo kwenye kifurushi hiki!
Kununua Zuku tv Tsh 88,000 bila ufundi! Ufundi ni Tsh 30,000! Piga +255 789 476 655
Niwe mkweli katika hili usipopata fundi makini uwezekano wa kuepuka hili ni mdogo sana vinginevyo muhusika uwe makini sana na Fundi wako ingawaje mara nyingi muhusika inakuwia vigumu kuona jinsi fundi wako alivyofunga Dish huko juu ya paa!!
Sababu zinazopelekea Dish kupata kutu kwa haraka:-
Sababu zisizoepukika:-
> Ikiwa Dish inafungwa ufukweni.
> Ikiwa Dish ni FAKE.
Sababu zinazoepukika:-
> Kutokuweka vinavyozuia maji kuingia.
Tuone madhara ya kutotumia vinavyozuia maji kuingia ndani na kukosa pa kutokea!
1
Hii ni Stendi ya kubeba Dish,hiki ni kikalio ( Chini ) ambapo kwa kutokufunika juu,imesababisha maji yameingia na kwakuwa hakuna sehemu maalumu ya kutokea maji yanapoingia,yenyewe yakatafuta njia kwa kutafuna kidogo kidogo mpaka kupata njia kama muonavyo!
2
Huu ni mkono wa kushika LNB,upo mfano wa V,mkono huu ni bomba maana yake kati lipo wazi,upande wa mbele inafungwa LNB ambapo inazima maji kuingia na upande wa nyuma kuna ya kukipachika ili kuzuia maji yasiingie kama ilivyoonyeshwa picha namba ( 5 ) kwakuwa yakiingia kinachotokea pale kwenye mkunjo ndipo maji yatajitengenezea njia kama muonavyo hapo juu!
3
Matokeo yake ile V inageuka vipande viwili baada ya kuliwa na kutu!
4
Ufungwaji Dish wa namna hii ndio unaopelekea madhara tuliyoyaona hapo juu kwenye picha ( 1 - 3 ) jinsi maji yalivyosababisha kutu,ambapo kama fundi angetumia vifaa vyote ipasavyo yasingetokea madhara hayo yaliyotokea!
5
Hivi ndivyo unavyopaswa kufunga Dish yako kwa kutumia Plastic cover ili kuzuia maji yasiingia kwenye bomba ya Stend na mkono wa kushika LNB!
Nadhani kwa uchache umeambulia kidogo kwa maelezo zaidi
Kwakuwa karibu Ving'amuzi vyote Tanzania vinatumia Dish ndogo leo niwape kasomo haka alau mwenye kujaribu na ajaribu atakapopata wasaa!!
Fanya haya ili uweze kufunga Dish ndogo:-
1.Dish Antenna Assembly:
- Unganisha kifaa kimoja kimoja kama karatasi ya maelekezi inavyoonyesha ili kulikamilisha dish lako bila kuacha hata kimoja kwakuwa kila kimoja kina kazi na umuhimu pia.
2.Unganisha stendi yako ya kubeba dish.
3.Angalia sehemu nzuri ya kufunga Dish ili uanze kufunga stendi yako:
- Hakikisha sehemu unayoifunga mbele hakuna miti itakayozuia kupokea signal.
- Sehemu imara itakayoweza kukaa Dish bila kucheza.
- Unashauriwa kuifunga juu ya usawa wa nyuma/jengo ili isipate kuguswa guswa.
4. Funga stendi yako ya dish sehemu ulipoona panafaa.
5. Funga Dish lako kwenye stendi kwa kulielekezea Satellite uliyoikusudia ( Muelekeo wa king'amuzi husika )
6. Unganisha Coaxial cable ( Signal cable ) kwenye king'amuzi chako kwa nyuma sehemu iliyoandikwa LNB IN kisha unganisha kwenye either kwenye Dish sehemu ya LNB ama kama utakuwa na kitafuta signal (Signal Finder ),kama utatumia Finder lazima uwe na Test cable ( Kipande cha cable ambacho utachomeka toka kwenye finder mpaka kwenye dish ( LNB ) - Nimetoa mfano wa Finder hii kwakuwa ni rahisi kupatikana na hata bei yake ni ya kawaida ila kuna finder nyengine hazihitaji Test cale.
7. Upo tayari kwa kuanza kutafuta signal. Jinsi ya kutafuta signal ntawaletea somo hilo katika post nyengine!