Tv ya kijerumani ya mwaka 1956
Neno "
televisheni" linatokana na maneno mawili:
tele (kutoka Kigiriki:
kwa mbali sana) na
visio (kutoka Kilatini:
mwono; kwa pamoja yanaunda neno la Kiingereza
television lililotoholewa katika Kiswahili
televisheni.
Televisheni -
TV au
runinga ni chombo (kifaa) chenye kiwambo au kioo ambacho kinapokea mawasiliano kutoka kituo cha televisheni na kuyabadilisha kuwa picha na sauti.
Kwa kawaida TV inaonekana kama sanduku. TV za zamani kabisa zilikuwa zina kirimba au fremu kubwa ya mbao na zilikuwa zikiwekwa chini kama fanicha. TV za kisasa ziko za namna nyingi kama zilivyo nyingi zaidi. Kuna baadhi ya TV zinaweza kuenea mkononi mwako zikawa zinaendeshwa kwa kutumia betri. TV nyingine zinaweza kuenea ukuta mzima wa nyumba, na inaweza kukaa katika sakafu, au kuna nyingine ambazo zimenyooka (flat) na zinaweza kubandikwa ukutani.
Televisheni inaweza kuonyesha picha kutoka sehemu mbalimbali. Cha kwanza unachotakiwa kufanya ni kutumia kidaka mawasiliano au antena (au aerial), hii itaonyesha yale yote yanayorushwa na kituo cha matangazo ya televisheni.
Vituo vya TV vinaweza kuwa mbali kabisa lakini bado matangazo yake yanapatikana kama antena ya kurusha mawimbi yake iko katika umbali wa kilomita 50 hadi 150. Teknolojia mpya zaidi ni kutumia vyombo vya angani kama antena ya kurusha mawimbi haya duniani. TV pia inaweza kuonyesha filamu kutoka katika VCD na DVD au VCR yaani tepu za kawaida. Cable TV na Satellite TV zinaweza zikatoa huduma nyingi za vipindi vya TV kwa mara moja na vilevile kuvirusha hewani. Michezo mingi ya video huunganishwa katika TV ili uweze kuona kile unachokicheza. Kuna baadhi ya tarakilishi au kompyuta ambazo unaweza kutumia TV kama kioo cha kufanyia kazi zako (kiwambo, au kwa jina lingine monita).
Baada ya Vita
Kuu ya II, mfumo bora wa utangazaji wa televisheni Black n White
ulikuwa maarufu nchini Marekani na Uingereza, na seti za televisheni
zilikuwa za kawaida katika nyumba, biashara na taasisi.Katika miaka ya 1950, televisheni ilikuwa katikati ya msingi kwa kushawishi maoni ya umma. Katikati ya miaka ya 1960, utangazaji wa rangi uliletwa nchini Marekani na nchi nyingi zilizoendelea.. Kawaida ya viwambo vingi (kioo au vioo) huonyesha kuwa vina kona ya mzunguko, lakini kwa sasa vioo vingi hutengenzwa kwa kunyooka na zina ncha pembeni.
Kabla ya miaka ya 1990, TV zote zilikuwa zikitengenezwa kwa umbo moja - zilikuwa kubwa kidogo na kisha zilikuwa ndefu. Kwa mfano, kama kioo kilikuwa cha urefu wa inchi 3, basi lazima kitakuwa na upana wa inchi 4. Au kama kioo kina urefu wa cm 30, lazima kitakuwa kina upana wa cm 40.
Umbo la TV za kisasa linazidi kuwa maarufu na kupata wapenzi wengi zaidi kila siku ziendapo. TV zenye kioo cha upana mkubwa wa mstatili
huonekana vizuri katika runinga kubwa (theatre screen) na pia
inapendeza wengi zaidi. Hizi huziita kioo kipana (widescreen). Endapo TV
ya kioo kipana ina urefu wa cm 30, basi lazima itakuwa ina upana wa cm
53. Ili ifanye kazi vizuri, uonyeshaji wa TV pia unatakiwa ujengwe kwa
namna ya upana yaani 'widescreen'. Kioo kipana kinaweza kubadilishika
kwa ukubwa wowote unaoutaka, lakini suala la umbo linabaki kuwa vilevile
kama lilivyo (widescreen).
Tangu mwaka
2010, kwa uvumbuzi wa smart television, internet television imeongeza upatikanaji wa programu za televisheni na sinema kupitia
mtandao kupitia huduma za video za Streaming kama vile Netflix, Amazon
Video, iPlayer, Hulu, Roku na Chromecast.
Aina za tv
Siku za usoni nitakuja kuzungumzia kwa kina kuhusu yaliyo hapa chini:
Broadcast Systems
- Terrestrial Television
- Cable Television
- Satellite Television
- Internet Television
Display Technologies
- Disk
- CRT
- DLP
- Plasma
- LCD
- OLED
- LDTV
- SDTV
- HDTV
- UHDTV
Imeandikwa na Mustapha Hanya
Whatsapp+255784378129