Call / WhatsApp +255673378129

Jan 21, 2018

STARTIMES KUWEKA CHANNEL ZA DSTV NA AZAM TV


Niliwahi kupata swali kama hili na nilishawahi kuona matangazo sehemu kadhaa mitandaoni ya kuwa kama unatumia king'amuzi cha Startimes tunaingiza channel za Azam tv na DStv na tangazo lengine kama unatumia king'amuzi cha azam tv unaingiziwa channel za DStv na Startimes pia....
Matangazo ni ya wengine lakini huwa nafatwa mimi ili kuthibitisha hili kwakuwa najua uthibitisho wangu ni msaada wa watanzania na wasio watanzania wengi sana..
Licha ya kuwa matangazo wanatoa wengine na namba zao ni nyengine tofauti na namba zangu, wanaotaka kuwahudumia wakiwabana zaidi kwa maswali ama ikitokea tofauti yeyote wanawaelekeza wapitie blog hii kwakuwa ndiye muhusika huyo huyo..
Huko nyuma niliwahi kulalamikiwa hili kwa wahusika kunihusisha na jambo hili ila kuna issue ilikuwa imenibana sana hivyo nikakosa muda wa kuandaa post na mwishowe nikawa kama nimekaa kimya ila nashukuru hivi karibuni kuna jamaa mmoja ambaye ni Fundi MaDish yeye anapatikana kawe, mambo ya ufundi kuzidiana ni jambo la kawaida sana na yeye alijua amezidiwa hivyo akataka kupata kitu ambacho yeye hakifahamu lakini katika kumbana bana ndipo jamaa akamuelekeza apitia kwenye blog hii ili apate ufafanuzi zaidi kwakuwa ndiye yeye maana yake ndiye mimi...
Kwa bahati baada ya kupitia humu akaona kuna utofauti mmoja wapo ni namba ya simu ndipo alipoona bora kunipigia kuendeleza yale maongezi lakini ikawa kama tunaanza upya hivi... ndipo akanieleza yoote..
UKWELI NI:-  Sihusiki na chochote kuhusu huduma hii ya kuingiza channel za Azam tv na DStv kwenye king'amuzi cha Startimes wala kuingiza channel za king'amuzi DStv kwenye Azam tv..
Hakuna huduma hii kama ambavyo wanatoa matangazo wahusika, asilimia 100 unaibiwa, ukituma pesa UMEIBIWA.
Wizi - Ikitokea imegundulika na DStv, Azam tv ama StarTimes unakamatwa wewe uliyewekewa ama unataka kuwekewa na yule muwekaji wa hizo channel. Wahusika wanaojitangaza wanatoa huduma hizi wanajua na ndo maana hawasemi wanapatikana wapi badala yake wanajifanya kumaliza kila kitu kwenye simu..



+255789476655
Insta @mustaphamadish
Share:

Jan 7, 2018

CHEAP CCTV CAMERAS INSTALLATION

Dunia imebadilika siku hizi ukiachilia umuhimu wa cctv cameras ni kupata ulinzi pia inakujuza kwa urahisi kinachoendelea muda ambapo wewe haupo na zuri zaidi unaweza ukapata kuona kinachoendea hata ukiwa nje ya nchi..
Tupo dar es salaam isipokuwa popote ulipo tanzania tunafanyakazi..
bei zetu ni nafuu sana..
wasiliana nasi kwa  Whatsapp+255784378129 / Call +255789476655
Insta @mustaphamadish


Share:

Jan 3, 2018

UNAZIJUA BEI NA OFFER ZA VING'AMUZI 2018!?


Biashara ushindani hivyo kuna maboresho kila kukicha kwenye swala la kukidhi haja za wateja na leo nakuletea list ya bei za ving'amuzi kwa mwaka 2017 na jinsi ya kununua kwa bei hii:-
  • Azam tv inauzwa Tsh 135,000/= Hii bila kifurushi wala Ufundi! Ila ina Offer katika malipo! Kwa maelezo zaidi Bofya Hapa
  • Digitek inauzwa Tsh .......
  • DStv inauzwa Tsh 79,000/=  Hii bila Ufundi ila ina Offer ya vifurushi vya miezi miwili! Kwa maelezo zaidi Bofya Hapa
  • Continental inauzwa Tsh .... ya Dish na Tsh 40,000/= ya Antenna. Hii bila ufundi ina Offer ya kifurushi cha miezi..! Kwa maelezo zaidi Bofya Hapa
  • StarTimes inauzwa ya Dish Tsh 78,000/= na ya Antenna Tsh 34,000/= Hii bila ya Ufundi ina Offer ya kifurushi cha miezi...! Kwa maelezo zaidi Bofya Hapa
  • Ting HD inauzwa ya Dish Tsh 100,000/= na ya Antenna Tsh 35,000 ina Offer ya kifurushi cha miezi..! Hii bila Ufundi Bofya Hapa
  • Zuku tv   inauzwa Tsh 88,000/= Hii bila Ufundi ila ina Offer ya kifurushi cha miezi...! Kwa maelezo zaidi Bofya Hapa 
  • NB: Bei zote zina mabadiliko kujua bei mpya check Whatsapp+255784378129
Zijue bei za vifurushi kwenye ving'amuzi kwa mwaka 2018 
Jinsi ya kuhama kifurushi
Kuepuka Dish lako kupata kutu
Kupata Mafundi Professional
Share:

Jan 2, 2018

BEI ZA VIFURUSHI KWENYE VING'AMUZI


Leo nakuletea bei ya orodha ya ving'amuzi ( Visimbuzi ) vyote Tanzania, pia utapata kujua idadi ya channels kwa kila kifurushi, naamini hii itakusaidia kujua kifurushi kipi ili ufanye malipo, ambacho naweza kukwambia liwe kama angalizo wakati unafanya malipo washa kwanza kisimbuzi chako, kisha ndipo ufanye malipo.
Chagua king'amuzi chako kwenye orodha kisha bofya itakupeleka mojakwamoja:-
Instagram natumia @mustaphamadish

Tumaini langu ni kwamba kwa uchache huu nimekurahisishia kitu, katika kutaka kujua bei na idadi ya channels.. Kama una Swali, Maoni, Ushauri ama chochote niandikie kwenye ukurasa wa Comment, nifollow instagram @mustaphamadish kama unahitaji private niandikie kwenye Email: mustaphamadish@gmail.com
Call/Text +255789476655
 
Share:

Jan 1, 2018

JE KOPO LINASAIDIA KIPINDI CHA MVUA!?

"Kwenye Kisimbuzi ( King'amuzi ) kinachotumia Dish kufunika lnb kwa KOPO hakusaidii chochote katika kufanya Kisimbuzi chako kisisumbue wakati wa MVUA..."
Tukirejea nyuma kidogo hata waliotengeneza SET ya dish waliangalia kama maisha ya dish ni ya kukutana na mvua na jua,hivyo wakatengeneza katika kuhimili hali zote mbili bila kushauri ama kuengeneza makopo ili yaweze kufunika lnb..
Binafsi lawama zangu kwa mafundi, kwa kuacha kutumia plastic cover ya lnb ambayo inasaidia kufunika coaxial cable inapofungwa kwenye lnb ili maji yasiweze kuingia kwenye lnb/cable na kusababisha short n.k. 

Kupata ushauri na mambo yote yanayohusu Visimbuzi tukutane Insta
@mustaphamadish Kupata MAFUNDI WA KUFUNGA VISIMBUZI/MADISH aina zote kwenye GUEST, LODGE, HOTEL, APARTMENT, OFFICE na MAJUMBANI kwa usafi na ubunifu wa hali ya juu, wasiliana nasi!
BAADHI YA SEHEMU TULIZOFUNGA NI:-

  • KING D HOTEL
  • TRANSIT MOTEL
  • JB BELMONT HOTEL
  • BONDENI HOTEL
  • TUCTA HQ
  • PSPF HQ
  • IKULU - OFFICE YA WAZIRI MKUU
  • JAMII FORUM OFFICE - Ilipokuwa sinza
  • CRDB BANK - mlimani city, Lumumba, Mikocheni n.k
  • DTB BANK - HQ n Magomeni branch
Uzoefu wa kazi ni zaidi ya miaka 10, tukisimamia kazi safi, 
bei nafuu na ubora ni zaidi ya wengine.
 
MAWASILIANO:-
Call/ Text 0789476655
Whatsapp +255784378129
Instagram @mustaphamadish
Share:

Dec 31, 2017

LNB NI NINI...??

Kwenye Technology kuna vifaa ambavyo kuvitafutia lugha ya kiswahili moja kwa moja hakuna ila nitakachojitahidi kufanya ni kukupa urahisi ili uelewe pasi kutoka nje ya maana yenyewe.



LNB ni nini?
LNB ama kwa kirefu chake ni Low Noise Block downconverter, ni kidubwana,kifaa kidogo kinachokaa kwenye dish ambacho kinapokea signal toka kwenye satellite na kupeleka kwenye satellite receiver ( King'amuzi kinachotumia dish ). Pia huitwa low-noise converter (LNC), au low-noise downconverter (LND), hiki kifaa wakati mwengine kinaitwa low-noise amplifier (LNA).

LNB ni mchanganyiko wa low-noise amplifier, frequency mixer, local oscillator na intermediate frequency (IF) amplifier. Inapokea microwave signal kutoka kwenye satellite iliyokusanywa na Dish, inaimarisha, na inachagua mzunguko wa mzunguko kwenye upeo wa chini wa mzunguko wa kati (IF). Hii downconversion inaruhusu signal kuletwa ndani kwenye Satellite receiver kwa kutumia Coaxial cable. ikiwa Signal ilibaki katika asili yake microwave frequency ingehitaji gharama kubwa na impractical waveguide line.

LNB kwa kawaida ni kisanduku kidogo kinachofungwa mbele ya uso wa dish kwa kutumia mfano wa fimbo ( kibomba/ vibomba ). Microwave signal kutoka kwenye dish inachukuliwa na  feedhorn kwenye LNB na hutolewa kwa sehemu ya waveguide.

LNB hufanyakazi kwa kutumia umeme ambao utatokea kwenye Satellite receiver kwa kutumia coaxial cable na huchomekwa sehemu iliyoandikwa LNB IN ikiwa imetumika pin katika kufanya coaxial cable kufunga kwenye Receiver na kwenye LNB pia.

AINA ZA LNB
  • Ku band 
  • Ka band
  • C band
Post hii itaendelea...
+255789476655
Whatsapp +255784378129

Share:

Dec 21, 2017

KUTUMIA KING'AMUZI KIMOJA KWA TV ZAIDI YA 1


Ving'amuzi vyote unavyovijua wewe iwe vya bure ama vya kulipia, nikiwa na maana vyenye kulipia malipo ya mwezi na visivyo na malipo ya mwezi, unaweza kutumia king'amuzi kimoja kwa tv zaidi ya moja, kwa kutumia king'amuzi kimoja unaweza kugawa picha kwa tv hata zikiwa 100.
Hii inawezekanaje!? kwanza unapaswa kujua ni king'amuzi gani ambacho unataka kugawa picha kwa tv zaidi ya moja,  chagua kwenye orodha hapo chini:-
NB:Nitaweka link kwa kila king'amuzi ambayo itakupeleka mpaka kwenye post ambayo itakuwa na maelezo yote kwa kina.
Kwa Maelezo zaidi hii hapa +255789476655
Whatsapp+255784378129
Share:

Dec 15, 2017

TELEVISION AU RUNINGA NI NINI!?

 Tv ya kijerumani ya mwaka 1956

Neno "televisheni" linatokana na maneno mawili: tele (kutoka Kigiriki: kwa mbali sana) na visio (kutoka Kilatini: mwono; kwa pamoja yanaunda neno la Kiingereza television lililotoholewa katika Kiswahili televisheni.
Televisheni - TV au runinga ni chombo (kifaa) chenye kiwambo au kioo ambacho kinapokea mawasiliano kutoka kituo cha televisheni na kuyabadilisha kuwa picha na sauti.
Kwa kawaida TV inaonekana kama sanduku. TV za zamani kabisa zilikuwa zina kirimba au fremu kubwa ya mbao na zilikuwa zikiwekwa chini kama fanicha. TV za kisasa ziko za namna nyingi kama zilivyo nyingi zaidi. Kuna baadhi ya TV zinaweza kuenea mkononi mwako zikawa zinaendeshwa kwa kutumia betri. TV nyingine zinaweza kuenea ukuta mzima wa nyumba, na inaweza kukaa katika sakafu, au kuna nyingine ambazo zimenyooka (flat) na zinaweza kubandikwa ukutani.
Televisheni inaweza kuonyesha picha kutoka sehemu mbalimbali. Cha kwanza unachotakiwa kufanya ni kutumia kidaka mawasiliano au antena (au aerial), hii itaonyesha yale yote yanayorushwa na kituo cha matangazo ya televisheni.
Vituo vya TV vinaweza kuwa mbali kabisa lakini bado matangazo yake yanapatikana kama antena ya kurusha mawimbi yake iko katika umbali wa kilomita 50 hadi 150. Teknolojia mpya zaidi ni kutumia vyombo vya angani kama antena ya kurusha mawimbi haya duniani. TV pia inaweza kuonyesha filamu kutoka katika VCD na DVD au VCR yaani tepu za kawaida. Cable TV na Satellite TV zinaweza zikatoa huduma nyingi za vipindi vya TV kwa mara moja na vilevile kuvirusha hewani. Michezo mingi ya video huunganishwa katika TV ili uweze kuona kile unachokicheza. Kuna baadhi ya tarakilishi au kompyuta ambazo unaweza kutumia TV kama kioo cha kufanyia kazi zako (kiwambo, au kwa jina lingine monita).
Baada ya Vita Kuu ya II, mfumo bora wa utangazaji wa televisheni Black n White ulikuwa maarufu nchini Marekani na Uingereza, na seti za televisheni zilikuwa za kawaida katika nyumba, biashara na taasisi.Katika miaka ya 1950, televisheni ilikuwa katikati ya msingi kwa kushawishi maoni ya umma.  Katikati ya miaka ya 1960, utangazaji wa rangi uliletwa nchini Marekani na nchi nyingi zilizoendelea.. Kawaida ya viwambo vingi (kioo au vioo) huonyesha kuwa vina kona ya mzunguko, lakini kwa sasa vioo vingi hutengenzwa kwa kunyooka na zina ncha pembeni.
Kabla ya miaka ya 1990, TV zote zilikuwa zikitengenezwa kwa umbo moja - zilikuwa kubwa kidogo na kisha zilikuwa ndefu. Kwa mfano, kama kioo kilikuwa cha urefu wa inchi 3, basi lazima kitakuwa na upana wa inchi 4. Au kama kioo kina urefu wa cm 30, lazima kitakuwa kina upana wa cm 40.
Umbo la TV za kisasa linazidi kuwa maarufu na kupata wapenzi wengi zaidi kila siku ziendapo. TV zenye kioo cha upana mkubwa wa mstatili huonekana vizuri katika runinga kubwa (theatre screen) na pia inapendeza wengi zaidi. Hizi huziita kioo kipana (widescreen). Endapo TV ya kioo kipana ina urefu wa cm 30, basi lazima itakuwa ina upana wa cm 53. Ili ifanye kazi vizuri, uonyeshaji wa TV pia unatakiwa ujengwe kwa namna ya upana yaani 'widescreen'. Kioo kipana kinaweza kubadilishika kwa ukubwa wowote unaoutaka, lakini suala la umbo linabaki kuwa vilevile kama lilivyo (widescreen).
Tangu mwaka 2010, kwa uvumbuzi wa smart television, internet television imeongeza upatikanaji wa programu za televisheni na sinema kupitia mtandao kupitia huduma za video za Streaming kama vile Netflix, Amazon Video, iPlayer, Hulu, Roku na Chromecast.
Aina za tv

Siku za usoni nitakuja kuzungumzia kwa kina kuhusu yaliyo hapa chini:
Broadcast Systems 
  • Terrestrial Television
  • Cable Television
  • Satellite Television
  • Internet Television
Display Technologies
  • Disk
  • CRT
  • DLP
  • Plasma
  • LCD
  • OLED
  • LDTV
  • SDTV
  • HDTV
  • UHDTV
 Imeandikwa na Mustapha Hanya
Whatsapp+255784378129
Share:

Dec 14, 2017

UTAJUAJE KAMA TV YAKO INA KING'AMUZI NDANI?


Swali la wengi kwasasa ni hili kutokana na ukweli kwamba uondoshwaji wa local channels kwa baadhi ya Visimbuzi imekuwa kama janga hivi.. Sasa niwape namna ya kujua jinsi gani ya kupata local channels kupitia tv ikiwa ina kisimbuzi ndani, inaweza ukatumia Antenna ama Dish inategemea na uwezo wa tv:-
Utajuaje kama tv yako ina kisimbuzi ndani?
  • Ingia kwenye INPUTs inategemea na brand, zipo ambazo zinatumia SOURCE, INPUT n.k unabonyeza na itakuletea orodha ya input zote mfano:-
AV
HDMI1
VGA
USB
ATV
DTV
Ukiona ina DTV ujue ina kisimbuzi.
  • Njia nyengine unachukua remote yako unabonyesha kwenye SETTING unaenda kwenye SEARCH hii nayo inategemea na tv, tv nyengine hutumia tune n.k hapa unaweza ukaweka AUTO SEARCH itakuletea Analogue tv na Digital tv ikikuletea hizo chaguo ujue tv yako ina kisimbuzi ila kama itakuletea Analogue tv pekee ujue haina kisimuzi..
 Ikiwa tv yako ina DTV maana yake inapokea matangazo ya Digital hivyo unapaswa kutafuta Antenna na kuchomeka muelekea wa Startimes/Ting ama Continental na kufanya search kama kila kitu kikiwa sawa channels zitaingia..
Kuna DVB T1/ T2 hii ni kwa ajili ya antenna.
Kuna DVB S1/ S2 hii kwa ajili ya dish.

Insta @mustaphamadish
Whatsapp+255784378129

Share:

Dec 13, 2017

UNALIPIA LAKINI INAKATA KABLA MWEZI KUISHA


Hii inaweza kutokea kwenye ving'amuzi vyote na hutokea makosa ya mtandao ama kama kifurushi ulichopo sio sahihi hivyo hakiwezi kufika mwezi kwa baadhi ya ving'amuzi! Mara chache mno hutokea kwa ving'amuzi kama cha Azam tv,DStv,Zuku, n.k. na huwa mara zote ni kufail kwa system tu na unachopaswa kufanya ni kutoa taarifa ili uweze kusaidiwa kwa kurudishiwa huduma. Tatizo hili limekuwa kubwa sana kwa upande waking'amuzi cha Startimes na huwa tofauti na ving'amuzi vyengine ili kujua zaidi Bofya hapa
Whatsapp+255784378129

Follow Insta @mustaphamadish
Share:

#FundiKalipua

Najivunia Tanzania yangu




Powered by Blogger.

Fanya kuni Follow Instagram

YOTE YANAYOHUSU VING'AMUZI TUKUTANE INSTAGRAM

Habari mdau wa Digital tv kiujumla! Najua alau kipo nilichowasaidia kupitia hii blog na wakati mwengine pengine siwasaidii kwa wakati na...

Nitumie Email

Name

Email *

Message *

Idadi ya Watembeleaji

Slider

FAHAMU KWA KINA: Kifaa kinachopokea matangazo ya Digital kinaitwa KISIMBUZI sio KING'AMUZI..

Culture

Wisata

Favourite

Event

Gallery

News Scroll

USHAURI | MSAADA KIUFUNDI | KUNUNUA PIGA/WHATSAPP +255673378129

Post zilizokupita